Januari
13,2016 Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza unawakutanisha Watanzania
katika Uwanja wa Furahisha uliopo katika Manispaa ya Ilemela Mkoani
Mwanza kwa ajili ya Maombi ya rasmi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi
wake ili kuliongoza Taifa vema.
Pia
maombi hayo ni mahususi kwa ajili ya kuliombea Taifa kwa ajili ya kupata
baraka mbalimbali. Kuanzia majira ya saa saba Wakazi wa Jiji la Mwanza
na maeneo jirani wameanza kujongea kwa ajili ya kujumuika pamoja katika
maombi hayo ambayo yatafikia tamati jioni.
Mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo huku wageni
mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini pamoja na waimbaji nyimbo za
injili wakihudhuria katika maombi hayo.
Picha na George Binagi.
SHARE








No comments:
Post a Comment