Mganga
Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Misasi, Ernest Msiba akikijaribu kimoja
kati ya vitanda 20 kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (watatu
kushoto) kumkabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Misungwi, Nathan Mshana (wapili kushoto). Waziri Kitwanga alikabidhi
vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka (20) kwa ajili ya Kituo cha
Afya cha Misasi pamoja na vitanda sita kati ya hivyo walikabidhiwa
Zanahati ya Nyamijundu iliyopo Kata ya Kasololo jimboni humo. Hafla ya
makabidhiano hayo ilifanyika katika Kijiji cha Misasi. Kushoto kwa
Waziri ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack
Bandawe, ambapo shirika lake pia lilitoa baadhi ya misaada katika kituo
hicho cha afya.
Meneja
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe (kushoto)
akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga, magaodoro (20) na
shuka (20) vyenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki tano katika
hafla iliyofanyika Viwanja vya Kituo cha Afya Misasi, wilayani Misungwi.
Waziri Chikawe baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo alivikabidhi kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, pamoja na vitanda (20)
vyenye thamani ya Shilingi milioni 16 ili aweze kuvigawa kwa Kituo cha
Afya cha Misasi pamoja na Zahanati ya Nyamijundu iliyopo Kata ya
Kasololo jimboni humo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akikata utepe wakati akifungua jiwe la
msingi la ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ihelele iliyopo Kata ya
Ilujamate, jimboni humo wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya
maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo. Waziri Chikawe
katika hotuba yake, aliwaahidi wananchi wa eneo hilo upatikanaji wa maji
hivi karibuni kwani eneo hilo linamradi mkubwa wa maji wa Mamlaka wa
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA), hivyo ni lazima maji yasambazwe kwa vijiji vyote vya jirani.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo
la Shule ya Msingi ya Ihelele iliyopo Kata ya Ilujamate, Wilaya ya
Misungwi. Shule hiyo inajengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na
kuchangiwa na Mamlaka wa Maji Safi na Usafi
wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) ambayo inamradi mkubwa wa maji
katika Kijiji cha Ihelele ambapo shule hiyo inapojengwa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya
Misasi mara baada ya kukabidhi vitanda (20), magodoro (20) pamoja na
shuka (20) katika Kituo cha Afya cha Misasi wilayani Misungwi. Waziri
Chikawe katika hotuba yake aliwaahidi wananchi wa eneo hilo ujenzi wa
barabara ya lami pamoja na upatikanaji wa maji.
Mkuu
wa Polisi Wilaya ya Misungwi (OCD), Sylivester Ibrahim akijibu maswali
ya wananchi wa Kata ya Misasi kuhusu usalama katika eneo lao. Ofisa huyo
wa Polisi alipewa nafasi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga
(kulia-aliyekaa) baada ya wananchi hao kutaka kujua masuala ya haki zao
waendapo Kituo cha Polisi kuripoti matukio mbalimbali.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kukabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vitanda (20), magodoro
(20) pamoja na shuka (20) katika Kituo cha Afya cha Misasi wilayani
Misungwi. Picha zote na Felix Mwagara.
SHARE
No comments:
Post a Comment