Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa
Singida Dk. Parseko Kone wakati alipowasili mjini Singida tayari kwa
maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa
kufanyika mjini Singida Jumamosi Februari 6 mwaka huu kwenye uwanja wa
michezo wa Namfua mkoani humo, wa pili kutoka kushoto ni Nape Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo na mkuu wa wilaya ya Singida mjini Mh. Said Amanzi.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi”
(PICHA NA JOHN BUKUKU – FULLSHANGWE-SINGIDA)
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa
Singida Dk. Parseko Kone wakati alipowasili mjini Singida tayari kwa
maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa
kufanyika mjini Singida Jumamosi Februari 6 mwaka huu mkoani humo,
kushoto ni Mh. Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM na
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na akina mama mbalimbali
waliojitokeza kumpokea wakati alipowasili mjini Singida jana.
Akina
mama na wana CCM mbalimbali wakiimba nyimbo za kumlaki Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili mkoani Singida jana. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment