Mitt Romney
Aliyekuwa
mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Mitt
Romney amekitaka chama chake kumkataa Donald Trump ,akimtaja mgombea
huyo aliye kifua mbele kuwa ''tapeli''.
Bwana
Romney amemshtumu Bwana Trump kwa kuwachukulia raia wa Marekani kama
wajinga katika hotuba ya siri iliotolewa kwa vyombo vya habari.
Bwana
Trump hatahivyo amemkejeli bwana Romney katika mtandao wa tweeter kama
mgombea aliyefeli na ambaye hafai kutoa ushari wowote kuhusu uchaguzi.
Viongozi
wakuu wa chama cha Reupblican wameshangazwa na vile bwana Trump
anavyoelekea kushinda tiketi ya chama cha Republican kwa uchaguzi huo wa
mwezi Novemba.
Donald Trump na Hillary Clinton
Inadaiwa
kuwa wanachama kadhaa wa kamati ya kitaifa kuhsu usalama wa jamii
waliandika barua ya wazi wakielezea maono ya bwana Trump kama yasio na
msingi wala sera.
Bwana
Trump amejiwasilisha kama muunganishi kufuatia ushindi wake katika
majimbo saba katika ile ilipotajwa kuwa jumanne maalum na hivyobasi
kuimarisha uongozi wake katika chama chake.
Romney
ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Trump anatarajiwa kutoa onyo katika
hotuba yake siku ya Alhamisi,kwamba sera za bwana Trump ni tishio kwa
chama cha Republican na taifa zaima kwa jumla.
Donald Trump
Bwana Romney pia ataonya kuwa uteuzi wa Trump utarahisisha harakati za Bi Hillary Clinton kushinda urais nchini humo.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment