Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akipokea maelekezo ya bidhaa kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya SLK Gold Taste wakati wa Mkutano na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius jana
Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa huduma za kibiashara wa
Tantrade, Fidelis Mugenyi (kushoto) na Balozi wa heshima wa Mauritius,
Abbas Rizvi.
Mkurugenzi
wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara
Odilo Majengo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Mkutano na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius jana Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Balozi wa heshima wa Mauritius, Abbas Rizvi (kulia) na Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah,
Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah akizungumza wakati wa mkutano na maonyesho hayo
Mkurugenzi wa TICC, David Lutabana akiongea wakati wa shughuli hiyo
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano huo.
Washiriki wa maonyesho wakitembelea baadhi ya wafanyabiashara
Serikali
imeahidi kuendelea kuboresha mazingira rafiki kwa wawekezaji ili
kuongeza miradi ya uwekezaji ili kufikia lengo na Dira ya Tanzania kuwa
nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Rai
hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijage
wakati wa ufunguzi wa Mkutano na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya
Mauritius yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili jana Jijini Dar es Salaam.
Alisema
moja kati ya jitihada zinazofanywa na serikali ni pamoja na matumizi ya
teknolojia ya habari na mawasiliano kufanya baadhi ya mambo ambapo sasa
usajili wa kampuni unaweza kufanywa mtandaoni.
“Natoa
wito kwa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Mauritius kuwekeza nchini
kutokana na uwepo wa rasilimali za kutosha, bandari pamoja na soko la
uhakika kwani nchi yetu inapakana na nchi saba ambazo muwekezaji anaweza
kuuza bidhaa huko kwa urahisi,” alisema Mh. Mwijage katika hotuba yake
iliyosomwa naMkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo.
Maonyesho hayo yanaandaliwa na kampuni ya Talemwa Investment Consulting Company (TICC) pamoja na Enterprise Mauritius kwa ushirikiano na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA).
Awali akiongea wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi
wa TICC, Bw. David Lutabana alisema maonyesho hayo ni fursa ya kipekee
inayowakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi hizi mbili ili kuweza
kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili fursa mbalimbali zilizopo katika
nchi hizo.
Akizungumza
wakati wa shughuli hiyo, Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius,
Rajen Subbamah, alisema sekta zinazoshiriki kutoka Mauritius ni pamoja
na sekta ya ukandarasi, bidhaa za kilimo, kemikali, viwanda vya
utengenezaji nguo na vidani, pamoja na sekta zingine.
“Nchi
yetu ina uhaba mkubwa wa malighafi na kwa upande mwingine Tanzania
imebarikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na rasilimali mbalimbali. Kupitia
mkutano huu tunatizamia kujenga mahusiano na wafanyabiashara wa hapa
Tanzania ili tuweze kufanya biashara zitakazonufaisha pande zote mbili,”
alisema Bw. Subbamah.
SHARE
No comments:
Post a Comment