Baraza la mawaziri la Ujerumani likiwa katika mkutano wake.
Baraza la
mawaziri la serikali kuu ya Ujerumani limepitisha hatua mpya siku ya
Jumatano zinazonuwia kudhibiti mmiminiko wa wakimbizi, zikiwemo kutaja
nchi zaidi salaama wanakotokea waomba hifadhi.
Muswada
wa sheria hiyo unahusisha pia kuanzishwa kwa vituo maalumu vya mapokezi
kwenye mipaka ambako maombi ya wahamiaji wanaotafuta hifadhi kutoka
mataifa yanayochukuliwa kusa salaama yanasguhulikiwa haraka na yumkini
kurejeshwa makwao.
Hatua
zilizotajwa katika pendekezo la muswada huo zitasitisha kuungana kwa
familia kwa muda wa miaka miwili, kwa wahamiaji ambao hawapati hadhi ya
moja kwa moja ya ukimbizi chini ya mikataba ya kimataifa, lakini ambao
wanaweza kukabiliwa na mateso iwapo watarudishwa nyumbani kwao.
Sheria
hizo ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na Merkel kuimarisha taratibu za
maombi ya hifadhi nchini Ujerumani, kuelekea uchaguzi muhimu wa majimbo
mwezi ujao.
AfD yatumia mgogoro kujiimarisha
Kura za
maoni zinaonyesha kuwa chama kinachopinga uhamiaji cha Alternative für
Deutschland - au Chama Mbadala cha Ujerumani, huenda kikafanya vizuri
katika majimbo ya Baden Würtenberg, Rheinland-Palatinate na Saxony
Anhalt.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment