Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiongea na Ujumbe
kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani). Ujumbe huo wa Washiriki
wa Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza
hapa nchini.
Wakufunzi
wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati yao
na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo
pichani). Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia
Jenerali, Jairos Mwaseba.
Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo
mafupi kwa Washiriki wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa
walipotembelea Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kwa ziara yao ya
Mafunzo(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna
Mwandamizi wa Magereza, Augustine Mboje.
Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo kutoka chuo cha Ulinzi wa Taifa wakimwangalia
mmoja wa wafungwa ambaye amepatiwa ujuzi gerezani wa kukata vitambaa vya
nguo tayari kwa kushona nguo za wafungwa wliopo magerezani kama
anavyoonekana katika picha katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Jijini
Dar es Salaam.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016(kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisalimiana na Mkufunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa ambaye ni raia kutoka China(katikati) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016.
SHARE
No comments:
Post a Comment