Timu za
Tanzania zinazoshiriki michuano ya Kimtaifa kwa ngazi ya vilabu ikiwemo
Azam na Yanga katika michezo yao jana Macho 12.2016 zimeweza kuchomoka
na ushindi ugenini hali ambayo zinajiweka katika nafasi nzuri ya
kusonga mbele zaidi kwenye michuano hiyo.
Yanga wao
wamweza kuchomoka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya wapinzani wao,
Warwanda, Klabu ya APRA ambayo ni ya Jeshi. Kwa upande wa Azam wao
wamepata ushindi huo jana usiku baada ya kuifunga bao 3-0 dhidi ya
wapinzani wao Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kombe la
shirikisho ikiwa ni saa chache baada ya Yanga kupata ushindi huo wa
magoli 2-1 dhidi ya APR Kigali, Rwanda.
Azam
walipata bao la kwanza lilifungwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya
50 baada ya kuachia shuti kali nje ya 18 kufuatia kona iliyopigwa na
Ramadhani Singano ‘Messi’ kuokolewa vibaya na mabeki wa Wits kisha mpira
kumkuta Sure Boy.
Dakika ya
57 baadaye, beki wa pembeni wa Azam FC Shomari Kapombe aliipatia Azam
bao la pili baada ya mabeki wa Wits kufanya uzembe kuokoa mpira kisha
Kapombe akaserereka na kupiga mpira uliotinga moja kwa moja kwenye kamba
za Wits.
John Bocco ‘Adebayor’ alihitimisha kipigo hicho kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 60 na kuiweka Azam kwenye mazingira ya kusonga mbele mbele kwenye michuano hiyo.
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 600w" alt="YANGAZ" width="702" height="467" style="display: block; margin-left: auto; margin-right: auto;" />John Bocco ‘Adebayor’ alihitimisha kipigo hicho kwa kufunga bao la ushindi dakika ya 60 na kuiweka Azam kwenye mazingira ya kusonga mbele mbele kwenye michuano hiyo.
Kikosi cha Yanga. Yanga wamepata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya APRA, nchini Kigali-Rwanda.
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 600w" alt="AZAM" width="702" height="517" style="display: block; margin-left: auto; margin-right: auto;" />
Baadhi ya
wachezaji wa Azam wakipongezana baada ya John Bocco kupachika bao
katika mchezo uliochezwa jana usiku Machi 12.2016, nchini Afrika Kusini.
Imeandaliwa na Andrew Chale, kwa msaada wa mashirika ya Habari.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment