Kampuni
ya wino na vifaa vingine vinavyotumika katika uchapaji ya Cartridge
World yenye makao yake makuu Hong Kong nchini China imezindua duka la
vifaa hivyo jijini Dar es Salaam lengo likiwa kusaidia kupunguza gharama
za uchapaji.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Cartridge World,
Rajesh Pandya alisema kuanzishwa kwa duka hilo nchini kutasaidia
kupunguza gharama za uchapaji kwani wino na vifaa vingine vya uchapaji
vya kampuni hiyo sasa vitapatikana kwa bei nafuu.
Alibainisha
kuwa kampuni hiyo itakuwa pia inatengeneza vifaa hivyo nchini vikiwa
katika ubora unaoitambulisha kampun I hiyo ulimwenguni ambako ina matawi
katika nchi 50 ulimwenguni na maduka zaidi ya 700 Marekani na 130
nchini Uingereza.
Alisema
unafuu wa bei utawezesha kushuka pia kwa gharama za uchapaji na hivyo
kuwapa nafuu wahitaji wa huduma za uchapaji na pia katika kuliepusha
Taifa na uharibifu wa mazingira, kampuni hiyo itakusanya vifaa
vilivyotumika hususan vya kuhifadhia wino na kuviteketeza.
Alisema
duka litrakuwa na matawi katika mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza kwa
kuanzia na wigo zaidi utapanuliwa ili kutosheleza mahitakji ya huduma za
Catrtridge nchini.
“Kifaa
cha kuhifadhi wino katia mashine ya uchapaji kikitupwa ardhini kinaweza
kuchukua hata miaka 400 hadi kuharibika hivyo kampuni yetu ulimwenguni
kote inakusanya vifaa hivyo vilivyotumika na kuziunda upya kabla ya
kuviingiza tena sokoni lengo likiwa kuepusha uharibifu wa mazingira”
alisema.
Awali
akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Mandeleo
ya biashara Kimataifa, Harry Stoubos alisema kufunguliwa kwa duka hilo
nchini ni njia ya kuingia katika soko la Afrika Mashariki na Tanzania
ndio nchi pekee ukanda wa Afrika Mashariki ambako duka linafunguliwa.
“Tanzania
ndio nchi ya kwanza Afrika Mashariki na tunatarajia kupanua wigo zaidi
katika ukandaa huu ili tuwe na martawi katia nchi zote za Afrika
Mashariki” alisema na kuongeza kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania
ndio ambayo imewavutia kuwekeza nchini.
Ofisa
Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni ya Cartridge,Harry Stoubos
(kushoto), akimkabidhi kabrasha Mkurugenzi Mtendaji wa Catridge
World-Africa Mashariki, Rajesh Pandya ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa
duka la vifaa kuhifadhia wino katika mashine za uchapaji vya kampuni
hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Cartridge World kwa Africa Mashariki, Rajesh Pandya na
Ofisa Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni hiyo,Harry Stoubos
wakionyesha kwa waandishi wa habari vifaa vya kuhifadhia wino katika
mashine za uchapaji wakati wa uzinduzi wa duka hilo, jijini Dar es
Salaam jana.
Meneja
wa Maendeleo ya Biashara –Afrika Mashariki wa Kampuni ya Cartridge
World, Ashish Nagewadia (kushoto), akifafanua jambo wakati wa uzinduzi
wa duka hilo. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji kampuni hiyo,
Africa Mashariki, Rajesh Pandya na Ofisa Mkuu Kimataifa, Harry Stoubos.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Cartridge World kwa Africa Mashariki, Rajesh Pandya (kulia)
na Ofisa Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni hiyo, Harry Stoubos
wakikata keki kuashiria uzinduzi wa duka hilo leo.
Ofisa
Mkuu wa Maendeleo Kimataifa wa kampuni hiyo, Harry Stoubos (kushoto)
akijadiliana jambo na Komal Nagewadia ambaye ni msaidizi mkurugenzi
mtendaji wa kampuni hiyo, wakati wa uzinduzi a duka hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment