Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Conrad Mselle akimfanyia usafi wa nywele mmoja wa watoto wanao lelewa
katika Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi waliopo Buhangija Mkoani
shinyanga walipofika katika kituo hicho kwa mwendelezo wa Wiki ya Afya
ya Kinywa na Meno ambapo kilele chake ni Machi 20, Mkoani Morogoro.
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA, MKOANI SHINYANGA, BUHANGIJA)
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad
Mselle akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno Mwanafunzi wa
Darasa
la pili Lucia Eliasi wa Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi
kilichopo Mkoani Shinyanga, Buhangija ambapo ni mwendelezo wa wiki
ya kinywa na meno duniani na kwa leo wameonwa watoto157 na kesho ni
mwendelezo wawale waliokutwa na matatizo.
Daktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga
Dk. Nuru Mpuya na akimwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.
Ntuli Kapologwe, akizungumza jambo, kushoto ni Kiongozi wa Msafara Dk. Arnold Mtenga
msimamizi wa Kituo cha Buhangija na Mwalimu wa Elimu Maalum na watoto
wasioona, Sasu Nyanga , akiwakaribisha Madaktari bingwa wa Afya ya
Kinywa na Meno
Daktari
Bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno wa Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera
akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Kituo hicho kwa Mapokezi na
uongozi huo kuboresha mambo waliyoyaomba mwaka jana yametekelezeka,
mfano,kuwekewa kituo cha afya ya kinywa na meno eneo hilo.
Mhudunu
wa Afya Mwandamizi, Scolastica Sawaki (kushoto) akimpatia Dawa ya
kujipata Esther Gada (kulia) mara alipofika katika Zahanati iliyopo
kituoni hapo , ambapo mwanafunzi huyo amefadhikiwa na Claire Grubbs
kutoka America na kufadhili mambo mengi shuleni hapo kwa kusomesha
baadhi ya watoto Veta wengine kwa lengo la kujifunza , Kutengeneza
Batic, ufundi wa Cherehani, utengenezaji wa sabuni, anaye shuhudia ni
Mhudunu wa Afya Mwandamizi wa kituoni hapo, Felister Jagadi
kiongozi
wa msafara kutoka katika hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Arnold
Mtenga, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa
akiushukuru uongozi wa kituo hicho kwa mambo muhimu waliyoyaomba
yafanyike na uongozi wa kituo umeteketeza na kuzidi kuwaomba mara wanapo
hitaji msaada kwa watoto haoa wasisite kutoa taarifa na wameonwa watoto
157
Baadhi wa watoto wakimlilia Mmoja wa Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno
SHARE
No comments:
Post a Comment