Mbunifu
wa mavazi, msanii wa filamu na mrembo maarufu nchini, Jokate Mwegelo
akimbeba mtoto aliyezaliwa siku ya wanawake duniani katika hospitali ya
Palestina jijini. Jokate alitembelea wodi hiyo na kutoa msaada.
Mbunifu
wa mavazi, msanii wa filamu na mrembo maarufu nchini, Jokate Mwegelo
akikabidhi moja ya msaada wake kwa mmoja wa mama aliyejifungua mtoto
wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika hospitali ya
Palestina jijini.
Mmoja
wa mofisa wa kampuni ya Suining Zerong Commercial Trading, Shuxia B
akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo. Kampuni hiyo inafanya kazi pamoja
na kampuni ya Kidoti.
Jokate
Mwegelo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya na mmoja wa maofisa wa
kampuni ya Suining Zerong Commercial Trading, Shuaijie Duan wakikabidhi
cheti cha shukrani kwa daktari mkuu wa hosptiali ya Palestina, Dk
Kariamel Wandi.
Mrembo
wa Tanzania namba mbili wa 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu
za kibongo, Jokate Mwegelo amewaomba wasanii wenzake na wadau wengine
kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma ya afya ya wazazi
na watoto.
Akizungumza
mara baada ya kutembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Palestina na
kutoa misaada mbalimbali kwa wanawake waliojifungua wakati wa
kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani, Jokate alisema kuwa
sekta hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi na kutokana na umuhimu wake,
wadau wanatakiwa kusaidia serikali.
Jokate
alisema kuwa serikali inafanya kitihada kubwa ya kuboresha sekta hiyo
na kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuelekeza nguvu na kufanikiwa
kutatua tatizo sugu lililokuwa linaisumbua la hospitali ya Taifa ya
Muhimbili T-scan matatizo kadhaa sugu katika.
“Kila
mmoja wetu anajua nini maana ya afya, huwezi kufanya jambo lolote kama
huna afya bora, hivyo matibabu bora ni muhimu, serikali inafanya vitu
vingi katika kuondoa kero za wananchi wake ikiwemo suala la afya,
nimeguswa na kuamua kuunga mkono kupitia kampuni yangu ya Kidoti ambayo
inazalisha viatu na nyewe,” alisema Jokate.
Alisema
kuwa amefuraishwa na huduma ya wodi ya wazazi ya hospitali ya Palestina
na ushirikiano waliopata kuanzia mganga mkuu wa manispaa ya Kinondoni
na uongozi wa hospitali hiyo kwa ujumla.
“Kama
unavyojua, misaada mingu uelekezwa kwenye hospitali kubwa kubwa tu,
kuna hospitali na zahanati nyingi ambazo zinahitaji kusaidia, hivyo
wasanii wenzagu, hii ni fursa kwenu kurudisha faida kwa jamii, si lazima
utoe fedha, hata kuwaona wagonjwa na kuwafariji,” alisema.
Alisema kuwa mikakati yake ni kuona anatembelea na kutoa alichonacho kwa hospitali na vituo vya afya mbalimbali nchini.
Mmoja
wa maofisa wa kampuni ya Kidoti, Shuxia Bi kutoka China alisema kuwa ni
vizuri jamii hasa wasanii wa muziki, filamu, warembo na wanamitindo
kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua matatizo kwa jamii yenye
mahitaji maalum. Shuxia alisema kuwa kupitia chapa ya Kidoti wanaamini
watafikia wadau wengi jijini nan je ya mkoa.
Dakitari Mkuu wa hospitali ya Palestina, Kariamel Wandi aliimpongeza
Jokate na kampuni yake kusaidia wodi ya wazazi. “Tumefarijika sana,
umeonyesha kuwa unajali, wengi wameshindwa kufanya kama unavyofanya
pamoja na kuwa na nafasi hiyo, naomba uwe na moyo huo huo,” alisema
Wandi.
Wandi
alisema kuwa Jokate amewasaidia wakati muafaka kwani hadi anakamilisha
kutoa misaada mbalimbali, jumla ya watoto 26 walizaliwa katika
hospitali hiyo. Kati ya hao, 18 ni wasichana na nane ni wavulana.
SHARE
No comments:
Post a Comment