Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana
jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii,
Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge
ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya
NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif. Kwa ujumla
Kamati ya Bunge imeridhishwa sana na utendaji mzuri wa Shirika la
Nyumba la Taifa na imeahidi kuyavalia njuga masuala ya Double Taxation
kwa serikali ili lifanyiwe kazi na Watanzania wengi zaidi wapate nyumba
za kuishi na suala la Mamlaka husika kufikisha huduma za kijamii katika
nyumba za NHC zinakojengwa kama za Maji, Umeme na Barabara. Picha Zote
kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha
NHC.
Mh.
Wilfred Lwakatare akiongozana na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula wakati Kamati hiyo ya Bunge
ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC
Mwongozo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda na
Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina
Mabula wakiwasili kwenye eneo la mradi wakati Kamati hiyo ya Bunge
ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC
Mwongozo.
Naibu
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula na
Mkurugenzi wa nyumba kutoka Wizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Michael Mwalukasa wakijadiliana jambo katika ziara hiyo
Wajumbe
wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa
Mikoa, Raymond Mndolwa wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara
katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Wajumbe
wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki, Hamad
Abdallah wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa
nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana
jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii,
Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge
ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya
NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif.
Mradi wa Mwongozo unavyoonekana kwa juu
Kamati
ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia
Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati
Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence
la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika
hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction
Limited.
Kamati
ya Bunge ikisikiliza maelekezo wa Mhandisi Anna Mrema anayesimamia
Jengo la Eco Residence kwa niaba ya NHC huku Naibu wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akifuatilia mazungumzo hayo wakati
Kamati hiyo ilipotembelea jengo la Nyumba za makazi za NHC Eco Residence
la Shirika la Nyumba la Taifa kujua utekelezaji wa miradi ya Shirika
hilo. Jengo hilo linajengwa na mkandarasi mahiri Estim Construction
Limited.
WAANDISHI WA HABARI KUTOKA NCHINI FINLAND WATEMBELEA TAASISI YA UONGOZI.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja (wapili
kutoka kushoto) akizungumza na kundi la waandishi wa habari kutoka
nchini Finland (hawapo pichani) mapema leo walipotembelea taasisi hiyo.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland
nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen, Mshauri wa masuala ya Ushirikiano
kutoka Taasisi ya UONGOZI Bi. Liisa Tervo na Mkuu wa Utafiti na Sera
kutoka Taasisi ya UONGOZI Bw. Dennis Rweyemamu.
Kundi
la waandishi wa habari 15 kutoka nchini Finland waliotembelea Taasisi
ya UONGOZI mapema leo ikiwa ni moja kati ya mafunzo yao katika programu
maalum ya maendeleo na sera inayoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya
Finland. Waandishi hao ambao wapo nchini kwa muda wa siku tano pia
walisindikizwa na watumishi wawili kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya
Finland.
Mratibu
wa programu ya Maliasili Bi. Namwaka Omari (kulia) akitoa mada kwa
waandishi hao wa habari kuhusu namna Taasisi ya UONGOZI inachangia
katika kuimarisha usimamizi wa maliasili zetu nchini hususan katika
sekta ya mafuta na gesi.
Mmoja
kati ya waandishi hao akiuliza swali. Baadhi ya mada zilizogusiwa
katika mazungumzo ni pamoja na jinsi gani Tanzania inatekeleza dhana ya
maendeleo endelevu, uimarishaji wa uwezo kwa viongozi barani Afrika,
uchumi wa sekta ya gesi nchini na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi ya
UONGOZI katika mazingira ya Serikali Mpya.
Mkuu
wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi.
Milma Kuttenen (kushoto) akitoa neno lake la shukrani kwa niaba ya
waandishi wa habari na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland,
walipotembelea Taasisi ya UONGOZI kufahamu shughuli zake mapema leo.
SHARE
No comments:
Post a Comment