Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuwasili katika ofisi za Mfuko wa Bima
ya Afya ya Taifa jijini Dar es salaam ambapo kamati hiyo imekutana na
uongozi wa mfuko huo ili kusikiliza mipango yao ya baadae na changamoto
mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio na
kuangalia mambo kadhaa yanayokwamisha shughuli za mfuko huo ili hatua za
kurekebisha zichukuliwe na kwa ajili ya kufanya mfuko huo kusaidia
jamii katika suala zima la afya , Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa mfuko
huo Bw. Michael Muhando.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES
SALAAM).
Mbunge
wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo
ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni na mbunge wa
Kigoma mjini Mh. Zitto Kabwe wakati wajumbe wa kamati hiyo walipowasili
katika ofisi za mfuko huo Kurasini jijini Dar es salaam.
Mbunge
wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo
ya jamii Mh. Raphael Chegeni pamoja na wajumbe wa kamati hiyo
wakiendelea na utaratibu wa kusaini kitabu cha wageni.
Wajumbe
wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakielekea mwenye
ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupewa taarifa na Kaimu Mkurugenzi wa
mfuko huo Bw. Michael Muhando wa kwanza kulia.
Kutoka
kulia ni Mbunge wa Ilala Mh. Azzan Zungu, Mbunge wa Kigoma Mh. Zitto
Kabwe, Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Busega Dk.
Raphael Chegeni, Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndugulile, Kaimu
Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya NHIF Bw. Michael Muhando na
Mkurugenzi wa huduma za utabibu na ufundi Dk.Frank Lekey wakielekea
kwenye mkutano.
Mbunge
wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo
ya jamii Mh. Raphael Chegeni akizungumza katika mkutano huo huku Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kigwangalla (katikati) akifuatilia mkutano huo, kulia ni mjumbe wa
kamati hiyo Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndungulile.
Wajumbe
wa kamati hiyo wakisikiliza wakati Kaimu Mkurugenzi wa NHIF alipokuwa
akiwasilisha ripoti ya shirika hilo kwa kamati hiyo leo.
Baadhi
ya wakurugenzi wa vitengo NHIF wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa
uwasilishaji wa ripoti hiyo mbele ya Makamti ya Bunge Maendeleo ya
Jamii, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani
Athumani na Ali Othman Mkurugenzi wa TEHAMA NHIF.
Mjumbe wa kamati Mbunge wa Buchosa Mh. Dk Charles Tizema akitoa mchango wake katika mkutano huo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo wakati wa
mkutano huo kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael
Mhando na katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati na Mbunge wa jimbo la
Buseka Dk. Raphael Chegeni.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk .
Mpoki Ulisubisya akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo huku wabunge
wakifuatilia.
Kaimu
Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa
yaliyojadiliwa na kamati hiyo pamoja na uongozi wa NHIF.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akikagua kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu
kilichoanzishwa kwa ajili ya kuwafanya wateja kupata taarifa mbalimbali
kuhusu mfuko huo bila kulazimika kufika ofisini.
Katibu
Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dk. Mpoki Ulisubisya akiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael
Muhando wakati akielekea kukagua eneo linaohifadhi kumbukumbu za mfuko
huo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).
SHARE
No comments:
Post a Comment