Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (mwenye suti nyeusi
kushoto), akiwatembeza Wajumbe wa Kamati Bunge ya Mauala ya Ukimwi
waliotembelea MSD Keko Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo ya Bunge ya Ukimwi, Hassna Sudi Katunda Mwilima (wa pili
kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe hao na wageni katika ziara hiyo.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (kulia), akiwatembeza wajumbe hao MSD Keko.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (katikati), akitoa maelekezo kwa wajumbe hao.
WAJUMBE
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI na dawa za kulevya
wametembelea Makao makuu ya Bohari ya dawa (MSD), Keko jijini Dar es
Salaam. Katika ziara yao kamati imeishauri serikali kutenga bajeti ya
dawa na vifaa tiba kulingana na mahitaji.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu asilimia 80% ya dawa kuagizwa nje ya nchi, Mkurugenzi
Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu amesema bado hakuna viwanda vya ndani
vya kutengeneza dawa ,na vichache vilivyopo havina uwezo wa kukidhi
mahitaji ya MSD.
Katika
hatua nyingine,wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge ya masuala ya
UKIMWI,inayoongozwa na Mhe.Hassna Sudi Katunda Mwilima(Mb.) imeipongeza
MSD kwa kuwa na maghala ya kisasa ya kuhifadhia dawa,huku wakihimiza
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ishughulikie
deni la serikali. Aidha, walisema kulipwa kwa deni kutasaidia MSD
kununua dawa muhimu kwa wakati.
Kuhusu
deni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya alieleza kuwa suala la deni linafanyiwa
kazi.
Hata
hivyo Naibu Waziri Dkt. Hamisi Kigwangalla amethibitisha kuwa tayari
serikali imeshaahidi kupunguza deni kwa awamu kuanzia mwaka huu wa
fedha.
SHARE
No comments:
Post a Comment