TRA

TRA

Thursday, March 17, 2016

Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini Wagawa vifaa vya kusomea, wafanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji kati ya wakulima na wafugaji wilayani kilosa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kilosa wakati alipokuwa akiongea nao walipotembelea shule ya palakuyo kutoa vifaa vya kusomea masomo ya Sayansi na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa.maafisa hao walitoa pia msaada wa vifaa vya kusomea masomo ya sayansi.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi.sylvia Lupembe(kushoto) akikabidhi vifaa vya kusomea masomo ya sayansi kwa mkuu wa wilaya ya kilosa Bw.John Henjewele wakati wakati wa kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akigawa msaada wa vitabu kwa watoto wa shule ya Mabwerebwere wilayani kilosa wakati walipotembelea walayani hapo kusaidia masuala ya elimu pamoja na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.
Mkurugenzi Idara ya Habari- MAELEZO Bw.Assa Mwambene(wa tatu kushoto) akikabidhi madawati kwa watoto wa shule ya msingi Tindiga wakati maafisa habari na mawasiliano wa serikali walipotembelea shule hiyo kugawa madawati na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji wilayani kilosa.Wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya kilosa Bw.John Henjewele(wa pili kulia). Picha na Daudi Manongi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger