Viongozi wa Umoja wa Ulaya na Uturuki katika mkutano Brussels
Viongozi
wa Úmoja wa Ulaya waanza mkutano wao huku mashaka yakianza kujitokeza
juu ya uwezekano wa kupatikana makubaliano na Uturuki.
Rais wa
halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean Claude Junker amesema anaimani
kwamba viongozi wa Jumuiya hiyo pamoja na Uturuki watafikia makubaliano
katika mkutano wa kilele wa siku mbili wenye lengo la kuutafutia
ufumbuzi mgogoro wa wakimbizi wanaomiminika barani Ulaya miongoni mwa
masuala mengine.
Kabla ya
kukutana viongozi hao mchana wa leo mjini Brussels Junker alikuwa na
mkutano na waandishi wa habari ambapo alizungumzia matarajio yake kwamba
anahakika makubaliano yatafikiwa kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki leo
au kesho. Juu ya hilo aliongeza kwamba anaamini makubaliano hayo
yataheshimu sheria za Umoja wa Ulaya na mkataba wa Geneva. Kwa upande
wake rais wa baraza la Ulaya Donald Tusk amesika akiwa na mashaka zaidi
kuhusiana na kikao hicho akisema.
''Makubaliano
ni lazima yakubalike kwa wanachama wote 28 wa Umoja wa Ulaya haijalishi
ni mwanachama mdogo au mkubwa.Pili makubaliano hayo lazima yazingatie
kikamilifu sheria za Ulaya na za kimataifa.Na tatu yanabidi yaweze
kusaidia kwa dhati kutatua mgogoro wa wakimbizi na kuchangia katika
mkakati wetu ambao ni pamoja na kuturudisha katika makubaliano ya
schengen na kumaliza wimbi hili kupitia sera,kutoa msaada wa kibinadamu
kwa Ugirikji kuziunga mkono nchi za Magharibi za Balkan na bila shaka
kuimarisha ushirikiano na Uturuki''(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment