Peter Magwi katibu wa Mbunge Jimbo la Tarime Mjini, Esther Matiko akikabidhi Mifuko ya Saruji Diwani wa Kata ya Turwa Zakayo Chacha Wangwe.
Diwani wa kata ya Turwa, Zakayo Wangwe akitoa Shukrani zake baada ya kupokea Mifuko ya Saruji kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko. |
Esther Matiko ni Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini Kupitia
CHADEMA na ni moja ya walioko katika orodha ya watoto wa Kike kutoka jamii ya
Wakurya aliyefanikiwa kupata Elimu akiwa mtoto wa Mkulima, Mhe Esther Matiko
amesema kuwa ataendelea kuinua Miundombinu ya Elimu ndani ya Jimbo lake.
Ikiwa ni sehemu ya Ilani yake ya
uchaguzi ya 2015 - 2020 katika kuhakikisha Jimbo la Tarime Mjini linafanikiwa
kuwa na Madarasa ya kutosha, Mhe Esther N. Matiko amewachangia Mifuko 30 ya
Saruji wananchi wa Mitaa ya Uwanja wa Ndege na Mkuyuni wanaojenga shule mpya ya
Mturu.
Kwa nguvu za Wananchi wa Mitaa hiyo
iliyoko Kata ya Turwa wamefanikiwa kujenga Maboma 6 yaliyofika usawa wa Lenta.
Mhe Esther N. Matiko katika
kuakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika mapema ili kuondoa hadha kubwa ya mrundikano
wa wanafunzi katika shule ya Msingi Rebu na kusababisha wanafunzi hao kusoma
kwa zamu amewachangia wanamitaa hiyo Mifuko 30 itakayotumika kufunga Lenta na
kujengea sehemu itakayokuwa imebaki kukamilisha ujenzi wa Maboma hayo.
SHARE
No comments:
Post a Comment