Kamishna
wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akizungumza na waandishi
wa Habari kuhusu matokeo ya uripuaji wa mabomu na kuchoma moto nyumba na
maskani za CCM Unguja na Pemba. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
Na Mwashungi Tahir na miza Kona – Maelezo Zanzibar
Nyumba ya
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa na
kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu na watu wasiojulikana majira ya saa
5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi
Kilimani, Kamishna Hamdani amesema tukio hilo limeathiri sehemu ya paa
la nyumba na dari na kujeruhi baadhi ya watu waliokuwa wamelala na
kusababisha hasara kubwa.
Amesema
tukio hilo linafanana lile lililotokea tarehe 03 mwezi huu katika
Maskani ya CCM Kisonge Unguja hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi
ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wanaofanya uhalifu huo.
Akizungumzia
matukio mengine ya uhalifu na kuchoma moto nyumba, maskani na kituo
cha Afya huko Pemba, alisema Jeshi la Polisi limeanza msako mkali na
kuwatia mbaroni watu 31 ambao wanaendelea kuhojiwa na watakaohusika
watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Kamishna
Hamdani amewatowa hofu wananchi kuhusu usalama wao na mali zao kuelekea
uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 20 mwezi huu na kuwepo kwa
ongezeko la askari katika maeneo mengi ya mijini na vijijini ni moja
ya juhudi za kuimarisha ulinzi na kuhakikisha uchaguzi huo utakuwa
salama na amani.
Ametahadharisha
kuwa mtu yoyote atakayejihusisha kuanziasha vurugu au kufanya kitendo
chenye ishara ya uvunjifu wa amani atapambambana na vyombo vya sheria.
Kamishna
Hamdani ametowa wito kwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura
kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya
kikatiba bila ya woga kwani jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi
sehemu sehemu zote.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment