Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema haitambui kujitoa kwa Chama cha
Wananchi (CUF), katika uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Kijitoupele hapa
Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Jumapili licha ya kuwa Tume imepokea
barua rasmi toka kwa uongozi wa Chama hicho.
Mkurugenzi
wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw. Kailima Ramadhani amesema Tume
imefikia maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF
imechelewa huku maandalizi ya uchaguzi huo yakiwa yamekamilika na ni
Wananchi tu kwa sasa Wanasubiriwa kwenda kupiga kura.
Aidha,
Bw. Kailima ameeleza kuwa, kwakuwa karatasi za kupigia kura
zilishachapishwa na kuwasili hapa nchini tayari kwa uchaguzi huo,
zitaendelea kuwa na picha za Wagombea wa CUF hata kama wamejitoa katika
uchaguzi huo.
Awali,
wajumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa
Tume Jaji mstaafu Hamid Mahamood Hamid walitembelea katika vituo
mbalimbali vya kupigia kura katika Jimbo la Kijitoupele ili kujiridhisha
na maandalizi ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili.
Tume
ilibaini kuwepo kwa baadhi ya kasoro ndogo ndogo katika baadhi ya vituo
vya kupigia kura ikiwa ni pamoja na kubanduliwa kwa karatasi zenye
majina ya wapiga kura, mfano katika kituo cha Skuli ya sekondari Kinuni.
Jimbo la
Kijitoupele lina jumla ya Wapiga kura wapatao 17,274 na vituo vipatavyo
53 vitatumiwa na wapiga kura ili kumchagua mbunge waJimbo la Kijitoupele
siku ya Jumapili.
Sambamba
na Uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele, marudio ya uchaguzi
mkuu wa Zanzibar Oktoba 25,2015 ambayo matokeo yake yalifutwa
uatafanyika Jumapili hiyo pia.
Uchaguzi
katika jimbo la Kijitoupele uliahirishwa mwaka jana kutokana na hitilafu
ndogo ndogo zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura, kabla ya
kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25,
2015.
Na Clarence Nanyaro(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment