Urusi
imesema jeshi lake liliopo Syria linajitayarisha kuondoka na kurudi
nyumbani kufuatia amri iliyotolewa na Rais wa Urusi Vladimir Putin,
baada ya kuanza kwa mazungumzo ya amani ya mzozo wa Syria mjini Geneva.
Taarifa
hiyo imetolewa siku moja baada ya Rais Putin kutoa amri ya kuondoka kwa
baadhi ya wanajeshi waliopo nchini Syria. Amri aliyoitoa siku yaliyoanza
mazungumzo ya amani yanayofanyika mjini Geneva.
“Ushirikiano
wa jeshi la Urusi pamoja na jeshi la Syria na vikosi vengine vya
kizalendo, vimefanikiwa kuleta mabadiliko makubwa na ya kushangaza
katika mapambano dhidi ya ugaidi wa kimataifa,” amesema Rais wa Urusi
Vladimir Putin.
Aidha
Putin ameongeza matumaini yake ni kwamba kujiondoa kwa jeshi la Urusi
itakuwa ni "ishara nzuri" kwa pande zote zinazopigana.
Kuanza
kwa mazungumzo hayo kunampa Putin nafasi nzuri ya kutangaza kusitisha
kampeni yake ya mashambulizi ya anga iliyoendelea kwa miezi mitano na
nusu nchini humo na ambayo ililisaidia kwa kiasi kikubwa jeshi la Rais
wa Syria Bashar al- Asaad kukamata baadhi ya maeneo muhimu nchini humo
na kujiongezea nguvu kabla ya kuanza mazungumzo.
Baadhi ya wanajeshi wa Urusi watasalia kuwepo
Hata
hivyo Putin ameweka wazi baadhi ya wanajeshi wa Urusi watabakia katika
kambi ya kijeshi ya eneo la Latakia pamoja na bandari ya Tartus nchini
humo. Aidha Shirika la habari la Syria limemnukuu Rais Asaad akisema,
Urusi itasitisha mashambulizi yake ya anga, lakini baadhi ya wanajeshi
wake watabakia nchini humo. Ikulu ya Syria imesema viongozi hao wawili
walizungumza kwa njia ya simu na kufikia aumuzi huwo.
Licha ya
kuondoshwa kwa baadhi ya wanajeshi wa Urusi, jeshi la Syria limesema
litaendelea na kampeni yake ya kuyashambulia makundi ya kigaidi, ya Dola
la Kiislamu-IS pamoja na la Al-Nusra.
Aidha
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakubaliana na uwamuzi
uliyochukuliwa na Urusi wa kuanza kuondoa wanajeshi wake nchini Syria.
Mashambulizi yaliyodumu miezi mitano na nusu
Urusi
ilianza mashambulizi ya anga nchi Syria mwezi Septemba kwa madai ya
kutaka kuliondoa kundi la kigaidi linalojiita dola la kiisilamu IS
linalodhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo, lakini kampeni hiyo ya kijeshi
kwa kiasi kikubwa ilikuwa na lengo la kumsaidia Rais wa Syria Bashar
al-Asaad.
Ingawa
Urusi imeweza imeweza kwa kiasi kikubwa kuingilia kati mapigano
yanayoendelea nchini Syria, wanadiplomasi wanasema hakuna hakika iwapo
itaweza pia kumshinikiza Rais Asaad kukubali kufikia makubaliano
yatakayoleta suluhu ya mgogoro huwo.
Katikaripoti
yake kwa wanachama wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mjumbe
maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Steffan de Mistura amesema kwamba
makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa Febuari 27, yanaweza
kuvunjika kirahisi na kwa maana hiyo yanahitaji kulindwa.
Mazungumzo
ya mjini Geneva, yaliyoitishwa na Umoja wa mataifa yalianza jana,
ambayo ni siku iliyotimia miaka mitano tokea kuanza kwa mzozo wa Syria,
ikiwa ni jitihada za hivi karibuni za kusitisha mapigano yaliyosababisha
vifo vya zaidi watu 270,000 na kupelekea mamilioni wengine kupoteza
mkaazi yao. DW(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment