
Wanajeshi wa Syria wakiwa na bendera ya nchi hiyo baada ya kuukombowa tena mji wa Palmyra. (27.03.2016)
Vikosi ya
serikali ya Syria vikisaidiwa na mashambulizi ya anga ya Urusi Jumapili
(27.03.2016) vimeukombowa tena mji wa kale wa Palmyra uliokuwa
ukishikiliwa ma kundi la Dola la Kiislamu tokea mwezi wa Mei.
Vyombo
vya habari vya taifa na shirika la uangalizi wa haki za binaamu vimesema
mji huo wa kale wa miaka 2,000 ambao ni turathi ya Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uko kwenye mikono ya
serikali baada ya mapigano makali yaliyodumu kwa wiki kadhaa.
Duru za
kijeshi zimeliambia shirika la habari la Ufaransa (AFP) kwamba "baada ya
mapigano makali ya usiku jeshi lina udhibiti kikamilifu mji wa Palmyra
ikiwa ni mji wenyewe wa kale na vitongoji vya wakaazi wa mji huo."
Shirika
la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la Syria limesema milio ya risasi
ilikuwa bado ikiendelea kusikika Jumapili katika eneo la mashariki ya
mji huo lakini wapiganaji wengi wa kundi la Dola la Kiislamu walikuwa
wameondoka kutoka mji huo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment