Timu ya
Taifa ya Wanawake Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Twiga Stars’ imetoka sare
ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ katika mchezo
uliochezwa jioni ya jana katika uwanja wa Rufaro jijini Harare.
Twiga
katika mchezo wa jana imecheza vizuri na kuweza kuwabana wenyeji katika
uwanja wao wa nyumbani kwa kuwalazimisha sare, na weyeji kupata nafasi
ya kusonga mbele katika hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 3-2.
Kwa
matokeo hayo Twiga Stars imetolewa kwenye michuano ya kuwania kufuzu kwa
Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa
mwaka huu nchini Cameroon.
Kikosi cha Twiga Stars kinatarajiwa kurejea nyumbani leo Jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Fastjet.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment