Kikosi
cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager kundi la kwanza limewasili salama jijini
D’jamena nchini Chad tayari kwa mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za
Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.
Taifa
Stars inayonolewa na kocha mkuu Charles Boniface Mkwasa akisaidiwa na
Hemed Morocco kimewasili D’jamena jana majira ya saa 7 mchana kwa saa za
huku kwa shirika la ndege la Ethiopia, sawa na saa saa 9 alasiri kwa
saa za nyumbani na Afrika Mashariki na kufikia katika hoteli ya Legder
Plaza.
Msafara
wa 20 wa kundi la kwanza uliowasili umejumuisha viongozi pamoja na
wachezaji 12, huku kundi la pili likitarajiwa kuondoka Tanzania Jumatatu
usiku na kuwasili Jumanne kuungana kwa mazoezi ya mwisho nchini humu.
Stars
inatarajiwa kufanya mazoezi kesho Jumatatu na Jumanne katika uwanja wa
Omnisports Idrissm Mahamat Ouya kujiandaa na mchezo huo wa Jumatano
katika dimba hilo hilo jijini D’jamena.
Wachezaji
waliowasili nchini ni Chad ni Ally Mustafa, Juma Abdul, Haji Mwinyi,
kelvin Yondani, Deus Kaseke, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Mwinyi
Kazimoto, Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na nahodha
Mbwana Samatta.
Mchezo
kati ya Chad dhidi ya Tanzania unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumatano
Alasiri kwa saa za huku, sawa na saa 11 jioni kwa saa za nyumbani
Tanzania.
SHARE
No comments:
Post a Comment