Mkurugenzi
wa Huduma za Ufundi Dawasa Mhandisi Romamus Mwang’ingo (Kushoto)
akitoa maelekezo kwa Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar
es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kulia) juu ya
ufanyaji kazi wa mitambo ya Ruvu chini.
Mafundi
wakiwa katika harakati za kulaza bomba litakalotumika kuleta maji
kwenye tanki kubwa lililopo kibamba toka Ruvu chini na juu kwa ajili ya
uhifadhi na usambazaji maji katika Jiji la Dar es salaam.
Mafundi
wakikarabati bomba kuu la kusambaza maji toka Ruvu juu katika
kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam
na maeneo jirani.
Mkuu
wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya
ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Katikati) akisikiliza maelezo juu ya
ufanyaji wa kazi wa mitambo inayotumika kusambaza maji toka Ruvu juu
kutoka kwa Meneja Mradi toka kampuni ya WABAG Mr. Pintu Dutta wakati wa
kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam ilipotembelea mitambo hiyo.
Mkuu
wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya
ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kushoto) akisikiliza maelezo juu ya ramani
inayoonesha usambazaji wa maji toka Ruvu Juu kwenda katika maeneo
mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za
Ufundi Dawasa Romamus Mwang’ingo.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Tatizo
la ukosefu wa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es
Salaam linatarajiwa kuwa historia mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa
tanki kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita million 10 kwa siku
lililopo Kibamba.
Hayo
yamebainika mara baada ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar
es Salaam walipotembela mradi huo unaofadhiliwa na nchi ya India ambapo
mbali na kujionea ujenzi wa tanki hilo pia walitembelea na kujionea
ulazaji wa bomba litakayokuwa linasafirisha maji toka vyanzo vya maji
vya Ruvu Chini na Ruvu Juu na kwenda kuifadhiwa katika tanki hilo tayari
kwa kusambazwa katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake.
Hata
hivyo Disemba 31, 2015 Serikali ya Tanzania na India zilisaini mkataba
wa ufadhili wa Dola Millioni 59.3 ili kutekeleza mradi wa ulazji wa
bomba la maji kutoka Mlandizi mpaka Kimara na kuishia Kinyerezi ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa tanki hilo la Kibamba.
Mradi
huo unatarajiwa kukamilika Marchi 31 mwaka huu ambapo mpaka sasa
umekamilika kwa asilimia 90 ili uanze kusambaza maji katika Mkoa wa Dar
es Salaam na viunga vyake.
Mkuu
wa msafara wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es Salaam alikuwa Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiq ambaye ndio mwenyekiti wa kamati hiyo
amesema lengo la kamati hiyo ni kuona Jiji zima linakuwa na huduma ya
maji safi na salama kwa matumizi mbalimbali na kuondokana na suala la
maji ya mgao linalolikumba Jiji la Dar es salaam kwa miaka mingi.
“
Tatizo la maji litakuwa historia katika Jiji letu maana mradi huu ni
mkubwa sana na utawezesha watu wengi kupata huduma ya maji safi na
salama na tutaondokana na uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo na yale
ambayo yalikuwa hayana kabisa huduma ya maji kwa kipindi kirefu sana
yatapatiwa huduma hiyo”
“
Nawaomba wananchi na wafanyakazi wa Dawasco kutunza miundombinu hii
kwani ni hazina kubwa si kwetu tu hata kwa vizazi vijavyo, na ni
marufuku kwa watu kujenga nyumba katika eneo lilipopita bombala maji,
alama maalum ziwekwe ili kuonesha kuwa sehemu hii bomba limepita ili
kuzuia uharibifu wa miundombinu” Alisema Mushi.
Mara
baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki la Kibamba litakuwa na uwezo wa
kusambaza maji katika maeneo yafuatayo; Ruvu, Kiluvya, Kibamba, Mbezi,
Kimara, ubungo, Segerea, hadi kinyerezi ambapo bomba linatakuwa
limeishia hapo na maeneo yote ambayo yanapata maji kupitia mtambo wa
Ruvu Juu na Chini na wale amabao bado hawajaunganishwa na huduma ya maji
wataunganishwa ili waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.
Aidha,
mmoja kati ya wajumbe wa kamati ya ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam
mbunge wa viti maalum Ilala (CHADEMA) Mhe. Anatropia Theonest amesema
huduma ya maji ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yoyote, hivyo
basi Serikali iliwekee uzito na kulitekeleza kwa nguvu zake zote na
kuonya wale wanaohujumu miundombimu ya maji kuchukuliwa hatua za
kisheria, iwe ni kwa wafanyakazi wa idara za maji au wananchi ili
kuhakikisha huduma hiyo inawanufaisha wananchi.
Kamati
ya ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam inaundwa na wakuu wa Wilaya zote za
mkoa wa Dar es salaam, Mameya wote, wabunge wa Mkoa wa kuchaguliwa,
kuteuliwa au viti maalum na kamati hiyo inakuwa chini ya Uwenyekiti wa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment