Waogeleaji wakichuana katika mashindano mbalimbali yaliyopita.
Na Mwandishi wetu
Jumla ya
waogeleaji 15 wa Tanzania (Tanzania Swim Squad) watashiriki katika
mashindano ya kimataifa ya Afrika Kusini yaliyopangwa kuanza Machi 28
mpaka Aprili 3 mjini Johannesburg.
Wachezaji
hao wametoka katika klabu tatu ambazo ni Dar Swim Club, Taliss na
Arusha ambao wataogelea kwa kutumia jina la Tanzania Swim Squad (TSS)
katika mashindano hayo ambayo yatafanyika kwa awamu mbili, yale ya
‘South Africa level 2’ na South Africa Level 1.
Mashindano
ya South Africa Level 2 yamepangwa kuanza Machi 28 mpaka Machi 31
kwenye bwawa la kuogelea la Ellis Park na yale ya South Africa level 1’
yaliyopangwa kuanza Machi 31 mpaka Aprili 3 kwenye bwawa la kuogelea la
Germiston.
Afisa
Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha aliwataja
waogeaji watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya South Africa level 2
kwa upande wa wanawake kuwa ni Marin de Villard, Celina Itatiro (Dar
Swim Club), Amani Doggart (Taliss), Josephine Oosterhuis, Jacqueline
Kortland na Isabella Kortland wote kutoka Arusha.
Kwa
upande wa wanaume ni Adil Bharmal na Pieter de Raadt kutoka Arusha.
Waogeleaji wa South Africa Level 1 kwa upande wa wanawake ni Ursula
Khimji, Anjani Taylor (DSC) na Slyvia Caloiaro (Taliss) na Kayleen Van
Rensburg wa Taliss wakati wanaume ni Dhashrrad Magesvaran, Harry
Mcintosh na Oliver Mcintosh wote kutoka Taliss.
Kwa
upande wa viongozi ambao wataambatana na wachezaji hao ni Inviolata
Itatiro, Thauriya Bharmal ambao ni wakuu wa msafara na makocha ni
Michael Livinstone, Alex Mwaipasi na Emma Mcintosh.
“BMT
imetoa kibali kwa waogeleaji hao kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika
mashidano hayo muhimu, waogeleaji hao wanatarajia kuondoka Jumamosi na
Jumapili, mchezo wa kuoegelea kwa sasa unakuja juu sana na lengo letu
ni kuona tunapata mfanikio kupitia mchezo huu, mashindano kama haya ya
kimataifa ni muhimu sana kwa waogeleaji wetu,” alisema Chacha.
Chacha pia alisema kuwa pia wameiruhusu waogeaji wa shule ya Braeburn ambao nao watashiriki katika mashindano hayo.
Katibu
Mkuu wa Dar Swim Club, Inviolata Itatiro alisema kuwa wanashiriki
mashindano hayo kwa mara ya pili na lengo lao ni kupata uzoefu wa
mashindano ya kimataifa.
“Haya ni
mashindano makubwa ambayo yatawashirikisha waogeaji kutoka nchi
mbalimbali Afrika, naamini Watanzania watajifunza na kupata uzoefu na
baadaye kutuletea medali katika mashindano mengine kama ya Olimpiki,
Jumuiya ya Madola na mashindano ya Dunia ya kuogelea,” alisema
Inviolata.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment