TRA

TRA

Thursday, March 24, 2016

Papa Mtakatifu aosha miguu ya waislamu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Papa Mtakatifu Francis
Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameosha miguu ya wahamiaji waislamu mjini Rome katika tukio la unyenyekevu linaloambatana na itikadi ya kuanza kwa msimu wa Pasaka.
Papa Francis alitembela makao ya wahamiaji, mjini Roma na kuendesha misa ya kuanza kwa msimu wa pasaka.
Ziara yake katika kituo hicho cha kutathmini uhalali wa wahamiaji cha (Castelnuovo di Porto), inawadia huku uhasama na taharuki ikienea kote barani ulaya kuhusiana na kuwepo kwa wahamiaji waislamu hususan kufuatia mauaji ya Paris mwezi Novemba na ya hivi punde huko Brussels Ubelgiji.
Papa Francis alikashifu mauaji yaliyotokea Ufaransa na Ubelgiji akisema kuwa hizo ni njama za watu wenye kiu cha kumwaga damu ya binadamu.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani alilaumu mtazamo wa watuhumiwa hao kuhusu maafa waliyosababisha.
Aidha papa mtakatifu aliwashauri watu wa dini tofauti duniani kuishi kwa amani.
''Haijalishi iwapo tunaimani tofauti la muhimu kwetu sote ni tuishi kwa amani sisi ni ndugu alisema papa mtakatifu.BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger