Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
BAADHI ya
wazazi wa wanafaunzi waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha St Joseph katika
matawi ya Arusha na Songea wametupa lawama kwa Tume ya vyuo vikuu
nchini (TCU) kwa hatua yake ya kufuta vibali vya kuanzisha matawi hayo
na kwamba hali hiyo imewathiri watoto wao.
February
26 mwaka huu ,tume ya vyuo vikuu ilitangaza kufuta kibali cha chuo
kikuu cha St Joseph (SJUIT) tawi la Arusha ikiwa ni wiki moja imepita
tangu kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo kwa Chuo kikuu cha St Joseph tawi
la Songea,vyuo vilivyoko chini ya shirika la kitawa la Dada wa Maria
Imakulata (DMI).
Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi
ya wazazi wameeleza kusikitishwa na hatua hiyo huku wakidai kuwaathili
kisaikolijia watoto wao ambao wengine walikuwa katika maandalizi ya
mitihani.
“Nadhani
ingekuwa ni jambo la busara kwa TCU kukaa meza ya mazungumzo na
uongozi wa chuo badala ya kuchukua hatua ya kukifutia vibali….Chuo hiki
kimekuwa kikitoa mchango mkubwa katika kuzalisha wataalumu mbali
mbali.”alisema Mrisho Sume.
Nchi
yetu ina wataalamu wachache katika sekta ya Sayansi na Teknalojia
,chuo hiki kilikuwa ni kimojawapo kinachotoa wataalamu hao hivyo mchango
wake unapaswa kuheshimika na kusaidiwa pale inapobidi,” aliongeza Sume
ambaye mwanaye alikuwa akisoma katika chuo cha Sayansi ya kilimo katika
chuo hicho tawi la Songea.
Mzazi
mwingine alijitambulisha kama Mariam Ali alisema taarifa alizokuwa nazo
ni kuwa uamuzi wa kufunga baadhi ya matawi hayo ulifikiwa bila ya
kukipa taarifa chuo hicho juu ya mapungufu yaliyopo ikiwa ni pamoja na
kukipa muda wa kuyafanyia kazi.
“Binti
yangu alikuwa akisoma tawi la Arusha na nimepata taarifa kuwa timu ya
ukaguzi kutoka tume ilifika chuoni hapo kwa ajili ya ukaguzi lakini
cha kushangaza ni kuwa chuo hakikupewa taarifa ya mapungufu
yaliyoonekana ili yafanyiwe kazi na badala yake kililetewa barua za
kufutiwa vibali.”alisema Mariam.
Uamuzi
ulifanywa ni wazi haukuzingatia haki na unatuumiza sisi wazazi pamoja
na watoto wetu, tulitegemea TCU kukipatia chuo ripoti ya mapungufu
waliyoyagundua na kupewa muda wa kuyafanyia kazi na endapo kingeshindwa
kuyafanyia kazi katika muda ambao kimepewa tume ingekuwa na haki ya
kutoa adhabu,” aliongeza Mariam.
Naye
John Budigle alisema tangazo lilitolewa na TCU kuhusu kufunga vyuo
hivyo lilisema moja ya matatizo yaliyopelekea kufungwa ni migomo ya
wanafunzi huku akiongeza kuwa migomo yote ilitokana na kucheleweshewa mikopo na siyo matatizo ya chuo .
“Mimi
kwa mtizamo wangu naona kama TCU imetumia nguvu kubwa kwenye suala
hili, kama chuo kilifanya makosa kilipaswa kupewa maelekezo ya
kushughulukia kasoro au mapungufu kwani hakuna chuo kisichokuwa na
mapungufu hata hivyo vya umma. “alisema Budigle.
“Hatua
hii inawavunja moyo wawekezaji katika sekta ya elimu. Hawa ni wadau
katika elimu na ni vizuri TCU wakatuchukuliwa hivyo. Wao ni wasimamizi
ambao wanatakiwa kuwaongoza na kuwarekebisha pale wanapokosea. Kitendo
cha kukifutia vibali bila kufuata haki kinawavunja moyo wadau wa elimu
pamoja na wanafunzi pia,” aliongeza Budigle.
Akitangaza
hatua hiyo hivi karibuni Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya,
alizitaja sababu za kufikia uamuzi huo kuwa ni matukio ya migogoro ya
muda mrefu baina ya uongozi wa chuo hicho na wanafunzi na ukiukwaji wa
sheria za uendeshaji wake kama ulivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu.
SHARE
No comments:
Post a Comment