TRA

TRA

Saturday, April 30, 2016

BASATA KUADHIMISHA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

New Picture
National Arts Council BASATA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Elimu na Sayansi (UNESCO) litaungana na wasanii mbalimbali nchini na wadau wa Sanaa kuazimisha siku ya muziki wa Jazz duniani ambayo kwa mara ya kwanza itaazimishwa nchini Mei 2, 2016.
Maazimisho hayo ambayo yatapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Wasanii wa muziki wa jazz hususan Band maarufu ya Das Jazz yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ofisi za BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Sambamba na burudani hizo, kutakuwa na mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wadau wa muziki huu wa jazz ambazo zitalenga kuamsha ari, thamani na ufahamu wa muziki huu maarufu duniani miongoni mwa wasanii nchini.
Wawasilishaji wa mada hizo pamoja na mada zao kwenye mabano ni pamoja na John Kitime (Matumizi ya neno Jazz), Carola Kinasha (Uhusiano kati ya Elimu ya Muziki na Jazz) na Kurwigira Mareges (Historia ya Muziki wa Jazz) na Masoud Masoud (Ujue Muziki wa Jazz)
Mbali na burudani na mada hizo kuhusu muziki huo wa Jazz kutakuwa na wageni waalikwa kutoka kwenye balozi na vituo vya Utamaduni vya nchi mbalimbali zilizopo hapa Tanzania
BASATA linatoa wito kwa wasanii na wadau wa muziki huu wa jazz kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya ambayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka sambamba na mataifa mengine duniani.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza
Katibu Mtendaji – BASATA (P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger