Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez
Ushindani
unazidi kupamba moto miongoni mwa kampuni za simu nchini ambapo katika
kipindi cha miezi mitatu cha kati ya Oktoba na Desemba mwaka 2015, ni
jumla ya watumiaji wapya 1,448,782 tu ambao walijisali kutumia huduma
zao za mawasiliano.
Ushindani
huu ambao umechochewa na kuingia kwa kampuni mpya katika sekta ya
mawasiliano Tanzania, umefikisha jumla kuu ya watumiaji wa huduma ya
mawasiliano nchini kufikia 39.8 milioni kwa mujibu wa
takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Mamlaka ya Mawasilano Tanzania,
(TCRA).
Kampuni
ya MIC Tanzania Ltd- ijulikanayo kwa jina lingine kama Tigo – ilisajili
juma ya wateja wapya 488,886 katika kipindi hicho cha miezi mitatu sawa
na asilimia 34. Idadi
hii ya wateja wapya inaifanya Tigo kuwa na jumla ya wateja 11,115,991
na kuifanya kampuni hiyo kuwa katika nafasi ya pili kwa ukubwa imiliki
asilimia 28 la soko la mawasiliano nchini na hivyo kuipita
Airtel ambayo imekuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha takriban muongo mmoja.
Airtel ambayo imekuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha takriban muongo mmoja.
Airtel
kwa upande mwingine ilisajili jumla ya wateja wapya wapatao 32, 839
katika kipindi hicho cha miezi mitatu na kufikisha jumla ya wateja wake
kuwa 11,047, 505 ambayo ni sawa na asilimia 28 lakini kiwa imezidiwa na
Tigo kwa idadi ya wateja 68,486. Licha
ya kuendelea kupungua kwa idadi ya wateja wake mwaka hadi mwaka, kwa
mujibu wa takwimu za TCRA, Vodacom bado inaongoza kwa kuwa na idadi
kubwa ya wateja wapatao 12,714,297 sawa na asilimia 32 ya jumla
ya watumiaji wote wa huduma za mawasiliano Tanzania.
ya watumiaji wote wa huduma za mawasiliano Tanzania.
Idadi ya wateja wa Vodacom imeonekana kushuka kutoka asilimia 45 mwaka
2007 hadi asilimia 41 mwaka 2008 na kufikia asilimia 39 Desemba 2009.
Wadadisi
wa sekta ya mawasiliano wanaelezea hali hii kushuka kwa idadi ya wateja
wapya miongoni mwa kampuni hizi kuwa kunachangiwa na mabadiliko ya
kimikakati ambapo msizitizo mkubwa miongoni mwa kampuni ni kuwalenga
Zaidi wateja watumiaji wa huduma za Intaneti kupitia simu zao
kama nyenzo kuu ya kukuza mapato tofauti na matumizi ya kuongea na
kutuma sms kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Meneja
Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez, kwa upande wake ameelezea kukua haraka
kwa kampuni hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kusema
kumechangiwa na sababu mbalimbali zikiwemo ubunifu mkubwa ambao
unafanywa katika kendesha kampuni kibiashara.
“Mafanikio
ya Tigo yameletwa na sababu nyingi kama vile kuwapa wateja wetu huduma
bora na kwa bei nafuu, upatikanaji wa mtandao wetu nchi nzima, utumiaji
wa teknolojia ya kisasa, ubunifu na kuwa karibu na wateja,” Gutierrez
anasema.
Akifafanua
Zaidi kuhusu ubunifu huo, Gutierrez ametaja baaadhi ya huduima na
bidhaa zilioanzishwa na kampuni hivi karibuni kama vile kuwapa wateja
uwezo wa kufanya miamala ya kibenki kupitia simu zao za mikononi, uwezo
wa kutuma na kupokea fedha kutoka mitandao mingine ya mawasiliano,
kutuma na kupokea fedha kimataifa na mgao wa faida utolewao kwa
watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa kila baada ya miezi mitatu.
Aidha meneja huyo mkuu ametaja vichocheo vingine vya kukua hara kwa Tigo kuwa ni “kubuni
huduma zinazolenga kuwapa wateja wetu fursa ya kuishi maisha ya kidijitali zikiwemo
huduma kama vile upatikanaji wa Facebook kwa lugha ya Kiswahili, simu zenye menu ya Kiswahili, WhatsApp ya bure na zinginezo,” amesema. Kampuni ya Tigo kwa mujibu wa Gutierrez inawekeza kiasi cha dola za kimarekani $ 120 milioni kwa mwaka katika kuboresha mtandao wake na kupanua upatikanaji wa huduma zake
nchini.
huduma zinazolenga kuwapa wateja wetu fursa ya kuishi maisha ya kidijitali zikiwemo
huduma kama vile upatikanaji wa Facebook kwa lugha ya Kiswahili, simu zenye menu ya Kiswahili, WhatsApp ya bure na zinginezo,” amesema. Kampuni ya Tigo kwa mujibu wa Gutierrez inawekeza kiasi cha dola za kimarekani $ 120 milioni kwa mwaka katika kuboresha mtandao wake na kupanua upatikanaji wa huduma zake
nchini.
Ametoa
mfano wa huduma ya 4G LTE ya Tigo ambayo kwa sasa inapatikana katika
miji sita – Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na
Mwanza – na kuelezea kuwepo kwa mkakati wa kufikisha huduma hii katika
mji mikubwa yote nchini ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Kwa
upande wake kampuni ya Zantel ambayo ni kampuni dada ya Tigo, zote kiwa
zinamilikiwa na Millicom, ilirekodi wateja wapya 320, 483 katika
kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ta mwaka 2015 na kufikisha jumla ya
wateja 1, 839, 391. Nayo kampuni mpya ya Haloteli ndiyo iliyoongoza
kwa kuvuna wateja wengi kipindi hicho wapatao 793, 383 na hivyo
kufikisha jumla kuu
ya waetja wake kuwa 1,226,678 hadi kufikia mwisho wa Desemba 2015.
ya waetja wake kuwa 1,226,678 hadi kufikia mwisho wa Desemba 2015.
Ikiwa
na wateja milioni 1.56 hadi kufikia mwishoni mwa Desemba 2015, Smart
ilikuwa na asilimia nne (4) la soko la mawasiliano ya simu nchini sawa
na Zantel wakati kampuni inayomilikiwa na serikali (TTCL) ikiwa
inashikilia asilimia moja (1) ya soko hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment