Mkuu wa Kitengo cha maradhi
yasiyoambukiza (NCD) Omar Mwalimu Omar akitoa elimu kwa wanafunzi wa
Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki juu ya njia bora za kujikinga na
maradhi yasiyoambukiza ikiwa ni maadhimisho ya siku ya afya Duniani.
Muuguzi kutoka kliniki ya
wagonjwa wa kisukari Hospitali ya Mnazimmoja Bi. Mwanaharusi Shaaban
akitoa elimu ya ugonjwa wa kisukari kwa wanafunzi wa Skuli ya
Mwanakwerekwe C katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afya Duniani
zinazoadhimishwa kila ifikapo tarehe 7 April. Zanzibar imeadhimisha
siku hiyo April 13 kwa kutoa elimu skuli za serikali na binafsi.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya
Mwanakwerekwe C wakimskiliza kwa makini mtoa elimu ya maradhi yasiyo
ambukiza Bi. Mwanaharusi Shaaban (hayupo pichani) wakati wa sherehe za
siku ya Afya Duniani zinazoadhimishwa kila ikifika tarehe 7 kila mwaka.
Mwanafunzi Shadia Issa Juma akiuliza swali kwa Muuguzi kitengo cha wagonjwa wa kisukari Bi. Mwanaharusi Shaaban.
Mkufunzi kutoka kitengo cha
maradhi yasiyoambukiza (NCD) cha Wizara ya Afya Rabia Ali Makame
akifundisha wanafunzi wa Skuli ya SOS kuhusiana na visababishi
vinavyopelekea maradhi yasiyo ya kuambukiza katika sherehe za
kuadhimisha siku ya Afya Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya
Mwanakwerekwe C wakimskiliza kwa makini mtoa elimu ya maradhi yasiyo
ambukiza Bi. Mwanaharusi Shaaban (hayupo pichani) wakati wa sherehe za
siku ya Afya Duniani zinazoadhimishwa kila ikifika tarehe 7 kila
mwaka.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
SHARE
No comments:
Post a Comment