Wanachama wa vuguvugu la Bring Back Our Girls waliandamana mjini Lagos Jumatano kutetea kuachiliwa kwa wasichana hao
Kanda ya
video iliyotumwa kwa maafisa wa serikali ya Nigeria kutoka kwa kundi la
wapiganaji wa Boko Haram inaonesha baadhi ya wasichana waliotekwa eneo
la Chibok wako hai.
Ni miaka miwili tangu kutekwa kwa wasichana 276 kutoka shule moja katika mji wa Chibok.
Ni wasichana 15 wanaoonekana kwenye kanda hiyo ya video ambayo inaaminika ilipigwa Siku ya Krismasi.
Video hiyo imepeperushwa hewani na shirika la utangazaji la marekani la CNN.
''Karibu niwe mlipuaji wa kujitoa mhanga''
Maafisa
wa Nigeria wamesema mashauriano kati ya serikali na wapiganaji hao wa
Kiislamu yanaendelea lakini yatasalia kuwa siri kwa sababu za kiusalama
na ili kuzuia wanaofanikisha wazungumzo hayo wasitambulike.
Mamake mmoja wa wasichana waliotekwa
Mwandishi
wa BBC aliyeko Abuja anasema video hiyo imewapa matumaini baadhi ya
raia wa Nigeria kwa sababu inaonesha baadhi ya wasichana wako hai.
Lakini
baadhi wanasema hali kwamba ni wasichana wachache sana waliooneshwa
kwenye video hiyo inaibua wasiwasi kuhusu hatima ya wasichana hao
wengine walioonekana kwenye video hiyo.
Kanda hiyo ya video ndiyo ya kwanza kutolewa ikiwaonesha wasichana hao tangu mwezi Mei mwaka 2014.
Serikali ya Nigeria imekosolewa kwa kushindwa kuwakomboa wasichana hao.
Shule ya Chibok inapatikana jimbo la Borno
Kwa muda mrefu, kitambulisha mada #BringBackOurGirls (Turejeshee wasichana wetu) kilivuma sana mtandao wa Twitter.
Mke wa
Rais wa Marekani Michelle Obama ni mmoja wa watu mashuhuri walioshiriki
katika kampeni ya kupigania kukombolewa kwa wasichana hao.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment