JAJI MKUU
wa Tanzania, Mohammed Chande Othman amesema sheria ya mitandao
ilipitishwa kwa lengo jema la kulinda watumiaji, wanajamii na usalama wa
Taifa la Tanzania.
Ametoa
kauli hiyo jana (Jumamosi, Mei 14, 2016) wakati akijibu baadhi ya
maswali kutoka kwa Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano
uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza.
Alisema
watu watatu kati ya wanne nchini Tanzania wakiwemo watoto, wanamiliki
simu za mkononi ambayo ni sawa na watu milioni 35 kati ya milioni 45.
Alisema
sheria hiyo ilitugwa kwa misingi mitatu moja ikiwa ni kumpa mtumiaji
uhuru wa kutoa maoni au taarifa, uhuru ambao alisema unalindwa kikatiba
lakini akaonya kuwa kila uhuru unaotolewa pia una mipaka yake kama
ilivyoainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Alisema
sheria hiyo pia inatoa uhuru wa mtu kuwa na faragha (privacy) na msingi
wa tatu ni sheria hiyo kuzingatia matumizi ya mitandao ili kulinda
usalama wa nchi.
“Sheria
hii inakupa uhuru wa kutumia mtandao kumlinda mwanajamii wenzako. Hapa
Uingereza nimeongea na mwendesha mashtaka mkuu ambaye aliniambia kuwa
asilimia 60 ya makosa yanayofanyika chini ya sheria ya makosa ya
kujamiiana (Sexual Offencea Act) yanatokana na mitandao,” alisema Jaji
Mkuu wakati akijibu swali kuhusu sheria ya makosa ya mitandao.
Naye
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga alisema kuitishwa kwa mkutano wa
kupambana na rushwa nchini Uingereza ni mojawapo ya jitihada za Waziri
Mkuu wa nchi hiyo kuanzisha vuguvugu la uanaharakati wa mapambano dhidi
ya rushwa.
“Kukosekana
kwa utawala bora, changamoto za ugaidi, biashara za dawa za kulevya,
biashara ya kusafirisha binadamu na uwepo wa rushwa na ufisadi ni baadhi
ya mambo yaliyofanya dunia ibadilike. Haya mambo zamani yalikuwa hayana
mahali pa kuzungumzwa, kwa hiyo vikao kama hivi vitasaidia kukabili
tatizo hili,” alisema.
“Rushwa
ni kama pweza mwenye vichwa vingi na mikia mingi. Waziri Mkuu David
Cameron ameamua kuanzisha movement hii ili kutafuta njia za kukabili
janga hili kubwa,” alisema.
Sote
tunatanbua kuwa mataifa mengi yangependa kuwemo katika hii movement
lakini ni faraja kuona kwamba Tanzania imo miongoni mwa waanzilishi na
hii ni kwa sababu ya uongozi nz ujasiri wa Rais Dk. John Pombe Magufuli
ambaye kwa kweli ni game changer (akimaanisha kuwa amebadili mwelekeo wa
Taifa hili) kwani ana utashi wa kisiasa na ana ujasiri wa kukemea
maovu,” alisema huku akishagiliwa.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola alisema
vita ya rushwa nchini Tanzania ni endelevu na inafanyika kuitikia wito
alioutoa Rais Magufuli wakati akizindua Bunge la Tanzania Novemba 20,
2015.
Alisema
wanatumia mbinu mbalimbali kupambana na rushwa lakini kubwa wanayoenda
nayo hivi sasa ni kutoa elimu kwa watoto na vijana ili kuwabadilisha
tabia na utamaduni uliojikita kwenye jamii.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment