Makala Kuelekea Miaka Kumi Ya Mjengwablog( Imezaliwa Sept 19, 2006)
Anaandika mwanazuoni Born Again Pagan ( BAP) kwenye mjengwablog/kwanzajamii
Msomaji,
kama umekuwa mfuatiliaji wa kuyasoma makala yangu haya ya kwanza,
napenda kukumbusha tu kwamba makala haya mpaka sasa yamekufafanulia kuwa
demokrasia ni utamaduni na mbinu (a technique) kwa madhumuni ya
kudhibiti utawala/uongozi wa mabavu au ki-imla au hali ya
utawala/uongozi wa bora liende; na sababu za kujifunza demokrasia kutoka
Amerika.
Zaidi,
yamekufafanulia kuwa wengine waliyafikiria ya Seneta Barack Obama kuwa
Rais Mweusi wa kwanza hapa Amerika kwamba yalitabiriwa; sifa za Seneta
Baraka Obama zilizofanikisha kampeini na kumletea ushindi; na jinsi
ubaguzi wa rangi ulivyoingilia mchakato wa kampeini.
Ninaendelea
na huo ubaguzi wa rangi katika makala ya leo, ikiwa ni pamoja na
kuonyesha endapo kizazi kipya cha wa-Amerika kimeachana na ubaguzi wa
rangi; ubaguzi miongoni mwa Weusi; na tamati fupi.
Tumeona
jinsi ambavyo Weusi wazito, hasa wa New York, walivyompigia debe Seneta
Hillary Clinton. Lakini Seneta Barack Obama hakukata tamaa. Aliinuka na
kusimama kidete kutetea kwa nini alikigombea u-Rais katika hotuba
aliyoitoa mjini Philadelphia, Pennsylvania, kwa wa-Amerika wote.
Alielezea kwa ufasaha hali ya ubaguzi wa rangi nchini Amerika. Wengi
waliipima hotuba hiyo na kuipa nafasi ya pili walipoilinganisha na ya
hayati Dk. Martin Luther King, Jr.: I Have a Dream!
Baadhi ya wa-Ulaya wengi walimwona Barack Obama kuwa ni Mweusi kutokana na kuwa na damu ya ki-Afrika.
Lakini
kuna wachambuzi wengine wa mambo ya uhusiano wa ubaguzi wa rangi ambao
wanaamini kuwa ubaguzi uliojitokeza kati ya wa-Amerika wenye asili ya
Ulaya, kwa upande mmoja, na wale wa asili ya Afrika, kwa upande wa pili,
ulikuwa ni wa kusutana tu. Haukuchimbua masuala yenye uzito mkubwa
yanayogusa maslahi ya wa-Amerika wenye asili ya Afrika na baadhi ya
mataifa mengine yasiyo ya asili ya Ulaya.
Kizazi kipya na ubaguzi wa rangi!
Kulingana
na takwimu aminika, wapigakura wengi waliomuunga mkono Seneta Hillary
Clinton walikuwa ni wa-Ulaya wenye zaidi ya miaka 50 hivi; waliamini
kuwa uwezekano wa Seneta Barack Obama kuchaguliwa ulikuwa nadra. Kundi
la Seneta Hillary Clinton likuwa ni la kizazi kizee – kundi la walio na
umri zaidi ya miaka 40!(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment