TRA

TRA

Tuesday, April 25, 2017

Afrika yahimizwa kuwekeza kwenye kilimo

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



ABIJAN, Cote d’Ivore

SERIKALI za Afrika zimehimizwa kuweka kipaumbele katika sekta ya kilimo ili kuharakisha maendeleo ya eneo hilo.

Pia imeelezwa kuwa ili kufanikisha suala hilo ni jambo jema kwa viongozi kujikita katika sekta hiyo ili kuleta mabadiliko chanya.

Hayo yalisemwa mjini Cote d’Ivoire wakati wa mkutano wa Baraza la Mabadiliko ya Kijani maarufu kama Green Revolution Forum (AGRF).
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini, Mamadou Sangafowa Coulibaly, alitaka nchi kuendelea kutimiza maazimio waliyojiwekea kuhusu sekta ya kilimo ya ziweze kupiga hatua kimaendeleo. 

 "Miaka mitano ya uwekezaji mkubwa umefanyika kupitia Mpango wa Taifa wa Kilimo cha Uwekezaji. Mpango huu umewezesha nchi kusaidia wakulima na kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi hapa hapa Côte d'Ivoire.

“Mpango wa kwanza ulilenga kusaidia uzalishaji sekta ya kilimo ambapo tani milioni 17 zilipatikana mwaka 2015 ukilinganisha na tani 11,886 mwaka 2012. 

“Tunapenda kuona jitihada hizi zinatambuliwa na jumuia ya kimataifa. Tunaamini awamu ya pili ya mpango huo utajikita katika masuala ya rasilimali maji, afya, umeme na elimu…hii itasaidia wakulima kuondokana na umaskini na kurutubisha uchumi wetu,”alisisitiza.

Aliongeza kuwa,” Côte d'Ivoire imedhamiria kwa moyo mmoja kuendeleza sekta ya kilimo kwani mchango wake ni mkubwa kwa nchi yetu,”. 

Akizungumza katika mkutano huo mjini Abidjan, Rais wa AGRA, Agnes Kalibata,   alisema:

“Kilimo ndiyo tegemeo kubwa kwa maendeleo ya nchi za Afrika katika kukuza uchumi”.
AGRF ni taasisi ambayo imedhamiria kuwekeza katika sekta ya kilimo ili kuleta mabadiliko chanya. 

Washirika wake ni pamoja na Umoja wa Afrika (AU), Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na taasisi nyingine nyingi.


 

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger