Shambulizi
baya kabisa, shambulizi la kujitolea muhanga kwa bomu lililotegwa ndani
ya gari, limelitikisa eneo linalokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia
la Sadr City kaskazini mwa Baghdad, na kuua watu 21.
Na RFI
Watu
wasiopungua 39 wameuawa Jumanne hii katika mfululizo wa mashambulizi
mapya yaliyotokea katika mji wa Baghdad. Hii ikiwa ni idadi ya muda
iliyotolewa na serikali ya Iraq. Mji wa Baghdad unashuhudia wiki ya pili
ya mfululizo wa machafuko.
Jumatano iliyopita, eneo linalokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia la Sadr City lilikumbwa na mashambulizi.
Kwa wiki
moja sasa, mashambulizi yamekua yakiendelea katika mji mkuu wa Iraq,
Baghdad. Mfumo unaotumiwa katika mashambulizi hayo ni mmoja: Mabomu
yanayotegwa ndani ya magari katika mitaa ya Baghdad au mshambuliaji wa
kujitoa mhanga analipua mkanda wenye kulipuka katikati ya soko, na hivyo
kusababisha watu wengi kupoteza maisha.
Jumanne
hii, maeneo matatu nchini Iraq yamekumbwa na mashambulizi haya, ikiwa ni
pamoja na kitongoji kikubwakinachokaliwa na watu kutoka jamii ya Mashia
cha Sadr City. Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na
mashambulizi haya, lakini kundi la Islamic State (IS) lilikiri kuhusika
na mashambulizi ya wiki iliyopita dhidi ya Mashia, wanaochukuliwa na
wanajihadi kama maadaui wa kwanza.
Wapiganaji
hawa wa "Khalifa" ambao wanasakamawa kwa mashambulizi ya anga ya
muungano wa kimataifa na vikosi vya Iraq waonekana kuwa wamebadilishwa
mkakati.
Mbali na mapigano katika uwanja wa vitai kunashuhudiwa kwa sasa ongezeko la mashambulizi ya kujitoa muhanga.
Tangu
kuanzishwa kwake kundi la Islamic State limefika mara kadhaa karibu na
mji mkuu wa Iraq. Lakini wapiganaji wake hawajawahi kuudhibiti mji wa
Baghdad. Njia pekee ambayo wamebaki nayo kwa kufikia mji mkuu, ni
mashambulizi ambayo mara kwa mara yamekua yakigharimu maisha ya wakazi
wa maeneo mbalimbali ya Iraq.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment