Kushoto
kwenda kulia, Waziri Mkuu wa Libya Fayaz al-Sarraj, Waziri wa Mambo ya
Nje wa Marekani John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Paolo
Gentiloni
Marekani
na nchi washirika zimesema zitaipatia silaha serikali ya Libya
inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa kulizuia kundi la Dola la
Kiislamu, IS na makundi mengine ya wanamgambo kujiimarisha kwenye ardhi
ya Libya.
Hayo
yamefikiwa katika mkutano uliomalizika usiku wa kuamkia leo mjini
Vienna, Austria. Nchi hizo hizo leo hii zinaendelea na mazungumzo kuhusu
mpango wa kumaliza vita nchini Syria.
Katika
tangazo la pamoja baada ya mkutano huo wa Vienna, nchi tano wanachama wa
kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, pamoja na nchi
nyingine zaidi ya 15 zilizoshiriki katika mkutano huo, zimesema
zitaridhia mauzo na misaada ya silaha kwa serikali mpya ya maridhiano ya
kitaifa ya Libya.
Nchi hizo zimesema ziko tayari kuitikia wito wa serikali hiyo, ambayo imeomba msaada wa mafunzo na vifaa kwa vikosi vyake.
Waziri Mkuu wa Libya atoa rai
Waziri
Mkuu anayeiongoza serikali hiyo Fayez al-Sarraj ambaye pia alikuwepo
mjini Viena, ameeleza sababu za kuutaka msaada huo. ‘'Tumeomba
tuondolewe vikwazo vya silaha, katika kuunga mkono jeshi na baraza la
ofisi ya urais katika kupambana na IS'' amesema al-Sirraj, na kuongeza
kuwa wameomba usaidizi katika kuandaa kikosi cha walinzi wa urais
walichokiunda hivi karibuni.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment