
Papa Francis akikutana na kiongozi mkuu wa chuo kikuu cha kiislamu nchni Misri Al-Azhar
Kiongozi
mmoja wa kidini nchini Misri amefanya mazungumzo na Papa Francis ,ikiwa
ni ishara za hivi karibuni za kutaka kuimarisha uhusiano kati ya dini
hizi mbili kubwa duniani.
''Mkutano
huu ndio ujumbe'', Papa Francis alisema,huku akikutana na Sheik Ahmed
el-Tayyib ,mkuu wa chuo kikuu cha kiislamu cha Al-Azhar na Msikiti.
Mkutano
huo unajiri miaka mitano baada ya Al-Azhar kusitisha mazungumzo na
Vatican kufuatia tofauti kubwa na aliyekuwa Papa Benedict wa kumi na
sita.
Mwaka
2006,Papa Benedict aliwashangaza Waislamu alipomnukuu kiongozi mmoja wa
Byzantine akisema kuwa baadhi ya mafunzo ya mtume Muhammad yalikuwa ya
''kishetani na yasio na utu'',madai ambayo Waislamu wanakana.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment