Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
SERIKALI
kupitia wakala ya Serikali mtandao imesema kuwa inaendelea kulifanyia
kazi suala la uanzishaji wa mfumo wa TEHAMA utakaowawezesha wananchi
kupata huduma na taarifa mbalimbali za Serikali kupitia simu zao mkononi
mahali popote walipo kwa njia ya mtandao.
Utaratibu
huo pia utawawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali vya elimu nchini
Tanzania kupata taarifa za ajira za Serikali na kuwawezesha kuomba
nafasi hizo, kufuatilia majibu ya usaili walioufanya na kupata taarifa
za kuitwa kazini kupitia namba za utambulisho watakazopewa kupitia
ujumbe mfupi (sms).
Akizungumza
na Wahariri wa vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu
wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) Dkt. Jabiri Bakari
amesema kuwa mfumo huo utamuwezesha mwananchi kupata huduma za
Serikali mahali popote alipo kufuatia mifumo ya TEHAMA kuwasiliana na
kubadilishana taarifa.
Amesema
kuwa dhana ya Serikali Mtandao ni kuwa na matumizi ya TEHAMA kwenye
shughuli zote za Serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguza
gharama za uendeshaji kwenye huduma za Afya, Utalii, Malipo ya tozo za
huduma,vibali, leseni ,elimu na huduma mbalimbali za Serikali.
Dkt.
Jabiri amesema moja ya vitu vinavyosababisha usumbufu kwa wananchi
kutokana na kukosekana kwa Serikali mtandao ni pale wanapohitaji kupata
huduma za Serikali ikiwemo Hati ya kusafiria ambapo hulazimika kwenda
Idara ya Uhamiaji kujaza fomu maalum na kisha kusubiri kwa muda wa zaidi
ya wiki moja ili taarifa zao ziweze kuhakikiwa na taasisi nyingine za
Serikali wakati suala hilo lingeweza kuchukua siku moja.
“Matumizi
ya TEHAMA kwenye shughuli za Serikali hurahisiaha sana upatikanaji wa
taarifa kwa kuwa mifumo inawasiliana na kubadilishana taarifa
haimlazimu mwananchi kwenda kwenye taasisi zaidi ya tano kupata huduma
yake” Amesisitiza Dkt. Jabiri.
Amesema
taasisi za Serikali kama Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji, RITA na taasisi nyingine ambazo
majukumu yao hutegemeana kupitia serikali mtandaomifumo ya taasisi hizo
huunganishwa ili ifanye kazi pamoja kwa lengo la kuruhusu mifumo
kuzungumza kumuhudumia mwanachi bila yeye kulazimia kuzifuata taasisi
hizo.
Amesema
kuwa pamoja na maboresho mbalimbali yanayoendelea ndani ya Serikali
ya kujenga Serikali mtandao imara mfumo uliopo sasa kwenye baadhi ya
taasisi humfanya mwananchi achukue muda mrefu kupata huduma.
Ameeleza
kuwa taasisi za Serikali zinazofanya kazi katika mazingira yanayofanana
zinaposhirikiana katika kutoa huduma Kupitia Serikali mtandao mwananchi
wa kawaida hatajua nini kinaendelea, atakachokipata mwisho ni majibu ya
huduma aliyoiomba kama ni Bandarini atachukua mzigo bila usumbufu
wowote kwa kuwa suala la kodi, upakuaji na upakiaji wa mizigo na ukaguzi
halitamgusa mwananchi.
Ameongeza
kuwa ili Serikali mtandao iweze kufanya kazi yake ipasavyo nchini
lazima kuwe na miundombinu ndani ya taasisi au nje pia uwepo wa mifumo
Tumizi ( Application Systems) inayoshughulikia masuala mbalimbali,
wafanyakazi pamoja na Sera, miongozo na taratibu za kusimamia
TEHAMA kuwezesha huduma mtandao ( e - Servieces).
Dkt. Jabiri amesisitiza Tanzania iko
kwenye hatua ya kwanza na ya pili, kwa maana ya taasisi nyingi za
Serikali zina tovuti zenye taarifa za awali za kumsaidia mtu kujua nini
kinapatikana au kutolewa na taasisi za serikali ili aweze kuchukua hatua
ya kupata huduma.
Amesema
Wakala ya Serikali mtandao imefanikiwa kuweka mifumo kwa maana ya
Tovuti kuu ya Serikali, Tovuti ya Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo
ina taarifa mbalimbali za wananchi kuhusu Maji, Barua pepe ya Serikali
(GMS) ambayo sasa inatumiwa na jumla ya taasisi 117 za Serikali na
Balozi mbalimbali kwa lengo kuepuka matumizi ya barua pepe za muda.
Amebainisha
kuwa Wakala ya Serikali Mtandao kwa sasa eGA katika awamu ya kwanza
imeziuganisha taasisi 75 za serikali na Wizara zote za Serikali kupitia
mkongo wa taifa, pia Wakala imeziunganisha Taasisi 72 zilizounganishwa
kwa simu zinazotumia itifaki ya Intaneti kwenye mkongo wa taifa ili
kurahisisha mawasiliano na kupunguza gharama.
Akijibu
Suala la baadhi ya Taasisi za serikali kukawia kuunganishwa kwenye
mtandao amesema kuwa awali hakukuwa na mfumo huo kutokana na baadhi ya
mapungufu yaliyojitokeza kwenye Sera, miongozo na taratibu zinazosimamia
utendaji wa shughuli za kila siku serikali lakini sasa kuna mwongozo wa
taasisi kuzingatia ili kuhakikisha mifumo ya taasisi za Serikali
inawasiliana ili kufanya kazi pamoja kuondoa mapungufu yaliyokuwepo.
Aidha,
mifumo ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea
kwenye taasisi hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa
makini sana kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo
likiwa kumhakikishia mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda
mfupi.
Kwa
upande wake Meneja Habari,Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan
Mshakangoto amesema kuwa suala la matumizi ya mitandao mbalimbali isiyo
rasmi katika shughuli za serikali linafanyiwa kazi huku akisisitiza
kwamba utaratibu unaandali wa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote ya
matumizi ya barua pepe nje ya zile za serikali kwenye ofisi za umma
yanafungwa kuanzia Saa 1:30 hadi saa 9:30.
Kwa
sasa ni taasisi 72 tu za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge na
taasisi zimeunganishw, Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo wa
taifa na kazi ya kuzifikia taasisi zote 500 inaendelea ili kuwezesha
zoezi la kufunga huduma za mawasiliano za serikali nje ya mkongo wa
taifa.
Takribani
taasisi 200 za umma zina tovuti ili kurahisisha upatikanaji wataarifa
na huduma kwa wananchi. Changamoto iliyopo ni Tovuti nyingi kukosa
taarifa zilizohuishwa pia kuunganisha maeneo ambayo bado hayajafikiwa
hasa Halmashsuri na vijiji ili kuwezesha taarifa mbalimbali kupatikana
kwa wakati.
Wakala
imepata mafanikio katika utekelezaji wa jitihada za Serikali mtandao
hasa katika uwekaji wa mifumo ya Serikali kwa maana ya Tovuti kuu ya
Serikali, Tovuti ya Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo ina taarifa
mbalimbali za wananchi kuhusu Maji, Barua pepe za Serikali ambayo sasa
ina taasisi 117 na Balozi mbalimbali zinatumia GMS ili kuepuka matumizi
ya barua pepe za muda.
Wakala
ya Serikali Mtandao katika awamu ya kwanza imeunganisha taasisi 72 za
serikali na Wizara zote za Serikali kupitia mkongo wa taifa pia
imeziunganisha taasisi hizo na simu zinazotumia itifaki ya intaneti
kwenye mkongo wa taifa ili kurahisisha mawasiliano na kupunguza gharama.
Akifafanua
kuhusu hatua ya mifumo ya serikali kuchelewa kufanya kazi pamoja
amesema hapo awali hakukuwa na mfumo uliowezesha jambo hilo kufanyika
kutokana na baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye Sera, miongozo na
taratibu zinazosimamia masuala ya TEHAMA nchini lakini sasa kuna
mwongozo uliotolewa kuhakikisha mifumo ya taasisi za Serikali
inawasiliana na kufanya kazi pamoja ili kuondoa mapungufu
yaliyokuwepo.
Aidha,
mifumo ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea
kwenye taasisi hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa
makini sana kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo
likiwa kumhakikishia mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda
mfupi.
Meneja
Habari, Mawasiliano Suzan Mshekangoto amesema suala la matumizi ya
mitandao mbalimbali isiyo rasmi katika shughuli za serikali linafanyiwa
kazi huku akisisitiza kwamba utaratibu unaandaliwa kuhakikisha kuwa
mawasiliano yote ya matumizi ya barua pepe nje ya zile za serikali
kwenye ofisi za umma yanafungwa kuanzia Saa 1:30 hadi saa 9:30 alasiri.
Amefafanua
kuwa taasisi 72 za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge na
Mahakama zimeunganishwa, Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo
wa taifa na kazi ya kuzifikia zilizobaki inaendelea ili kuwezesha
mawasiliano ya serikali kupita kwenye mkongo wa taifa.
SHARE
No comments:
Post a Comment