Mwanadiplomasia
mkuu wa Ujerumani ametupilia mbali madai kwamba serikali imekuwa
ikiiridhia mno Uturuki kwa ajili ya kutaka kutekelezwa kwa makubaliano
tata ya wahamaji kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya.
Katika
mahojiano na gazeti la Ujerumani la "Der Spiegel " yaliochapishwa
Jumapili (15.05.2016) waziri wa mambo wa Ujerumani Frank- Walter
Steinmeier amekanusha kwamba serikali ya Ujerumani imekuwa ikijaribu
kuiregezea Uturuki wakati wa kujadiliana nayo masuala magumu kwa kuhofia
kuvuruga makubaliano ya wahamiaji kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya.
Ameliambia
gazeti hilo kwamba "Tuatendelea kuzungumzia matukio yanayokwenda
kinyume na inavyostahiki nchini Uturuki,kuhusu vikwazo dhidi ya uhuru wa
kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari."
Uturuki
katika meizi ya hivi karibuni imekuwa ikikabiliwa na shutuma kali kwa
kuwachukulia hatua za kisheria waandishi wa habari wenye kuandika
habaria za kisiasa kwa mtazamo wa kukosowa serikali na kuwazuwiya
waandishi wa habari wa kigeni nchini humo.
Kama
sehemu ya makubaliano yake na Umoja wa Ulaya yaliofikiwa mwezi wa Machi
serikali ya Uturuki imekuwa ikiwazuwiya watu wanaowasafirisha wakimbizi
na wahamiaji kwa magendo kuutumia mwambao wake kuwaingiza katika ardhi
ya Umoja wa Ulaya kwenye visiwa vilioko karibu vya Ugiriki.
Mpira uko kwa Uturuki
Steinmeier
amesema maslahi ya Uturuki katika makubaliano hayo yasidharauliwe
ambayo yataipatia Uturuki zaidi ya euro bilinioni 3 kudhibiti wimbi la
wahamiaji na wananchi wa Uturuki kusafiri bila ya viza katika nchi za
Umoja wa Ulaya.
Amesema
masharti ya Umoja wa Ulaya kwa Uturuki kuregezewa upatikanaji wa visa
kwa wananchi wake yanatambuliwa na serikali ya nchi hiyo kwa kuwa
yamejadiliwa pamoja na serikali hiyo na kuongeza kuwa "mpira sasa uko
upande wa Ututuki".(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment