Thursday, June 30, 2016
Kampuni ya Nation yafunga vituo vyake
Jumba na Nation mjini Nairobi
Kampuni kubwa zaidi ya Habari Afrika mashariki, Nation Media Group, imeamua kufunga baadhi ya vituo vyake.
Hatua hiyo itashuhudia idadi kubwa zaidi ya watu kupoteza kazi zao.
Katika
taarifa iliyopokelewa nchini Kenya, NMG kama inavyofahamika, imeamua
kufunga vituo kadhaa vya Radio kama vile Nation FM, QFM na KFM iliyoko
Kigali nchini Rwanda.
Mbali na vituo hivyo vya Radio, itafunga pia kituo chake kimoja cha Runinga QTV.
Nation Media Group inasema sasa itaelekeza juhudi zake kuboresha taarifa za mitandaoni.
Kampuni hiyo ilianzishwa na muathama Aga Khan yapata miaka sitini iliyopita.BBC
Tishio la Dola la Kiislamu lainyemelea Kenya
Imebainika
kwamba kwamba ushawishi wa kundi la Dola la Kiislamu Afrika Mashariki
umeongezeka kwa kuwaandikisha vijana wa Kenya kuendesha mapambano ya
jihadi nchi za nje na baadhi yao kurudi Kenya kuitishia nchi hiyo.
Mashirika
ya ujasusi nchini Kenya yanakadiria kwamba takriban wanaume na wanawake
100 yumkini wakawa wamekwenda kujiunga na kundi la Dola la Kiislamu
nchini Libya na Syria na kuzusha wasi wasi kwamba baadhi yao huenda
wakarudi nchini humo kufanya mashambulizi kwa Kenya na katika vituo vya
kigeni, katika nchi ambayo tayari ni muhanga wa mashambulizi ya kigaidi
yanayofanyika kila mara nchini humo.
Rashid
Abdi mchambuzi mwandamizi katika Shirika la Kimataifa la Kushughulikia
Mizozo ambalo ni jopo la ushauri lilioko katika mji mkuu wa Kenya
Nairobi amesema "kwamba hivi sasa kuna tishio la kweli linaloikabili
Kenya kutoka kundi la Dola la Kiislamu na hatari hiyo itazidi
kuongezeka."
Tatizo la
wafuasi wa itikadi kali ambao mara nyingi ni watu wenye shauku lakini
wasiokuwa na mafunzo, kupatiwa mafunzo stadi ya kigaidi na kundi la Dola
la Kiislamu na kurudi nyumbani kufanya mashambulizi ni tatizo ambalo
tayari mataifa ya Ulaya yanakabiliana nalo na yumkini hivi karibuni
likawa pia ni tatizo kwa Kenya.
Mshauri
elekezi wa masuala ya usalama na afisa polisi wa zamani George Musamali
ameliita hilo kuwa ni "bomu linasubiri kuripuka."Amesema watu kwenda
Libya au Syria sio tatizo kwa Kenya tatizo ni kile watakachokifanya
wakati watakaporudi.
Mashambulizi ya kigaidi sio tu kigeni Kenya
Shambulio
la kwanza la kigaidi la Al- Qaeda nchini Kenya ilikuwa ni kuripuliwa
kwa ubalozi wa Marekani hapo mwaka 1998 na hivi karibuni kabisa yalikuwa
ni mauaji katika chuo kikuu cha Garissa mwaka jana lakini tishio la
Dola la Kiislamu ni jipya na bado kueleweka vyema.
Hapo
mwezi wa Machi wanaume wanne walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za
kutaka kwenda Libya kuijunga na kundi la Dola la Kiislamu.
Baadae
hapo mwezi wa Mei polisi ya Kenya ilitangaza kukamatwa kwa mwanafunzi wa
udaktari,mke wake na shoga yake wanaotuhumiwa kuwaandikisha watu
kujiunga na kundi la Dola la Kiislamu na kupanga shambulio la kibiolojia
kwa kutumia anthrax.
Inasemekana wanafunzi wengine wawili wa udaktari wamekimbia.
Kukamatwa kwa silaha
Wiki tatu
baadae polisi ya Kenya ilitangaza kukamatwa kwa wanachama wengine
wawili wa mtandao wa kundi la Dola la Kiislamu ambao ulikuwa ukitaka
kujipenyeza Kenya ili kuweza kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya
Wakenya wasiokuwa na hatia.
Polisi
ilisema imegunduwa vitu ambayo hutumiwa na magaidi kutengeneza mabomu ya
kienyeji pamoja na mikuki na mishale iliotiwa sumu.
Wakati
baadhi ya wataalamu wanatupilia mbali ishara ya shambulio kubwa
lainyemelea Kenya wanakiri kwamba kuna tishio la dhati la kundi la Dola
la Kiislamu kupandikiza itikadi kali,kuandikisha watu kujiunga nalo na
baadae kuwarudisha nyumbani.DW
MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva katika mazungumzo kati yake na wajumbe wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyofanyika kwenye makazi yake mjini
Dodoma Juni 30, 2016.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva katika mazungumzo kati yake ya Wajumbe wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaliyofanyika kwenye makazi yake mjini Dodoma
Juni 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wa
Rais na Wabunge wa 2015 kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Tume ya taifa ya
Uchaguzi kwenye Makazi yake mjini Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi baada ya kuzungumza nao kwenye makazi yake mjini
Dodoma Juni 30, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji
Damiana Lubuva.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(P.T)
Dkt. Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Loiuse Mushikiwabo, alipomtembelea leo katika
Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika
kuimarisha na kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili,
pamoja na Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame
anayetarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku mbili.
Kaimu
Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Bw. James Bwana alipokuwa akimkaribisha Mhe. Waziri
Mushikiwabo mara baada ya kuwasili Wizarani.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Samuel Shelukindo, akiwa
na Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana na Afisa Mambo ya Nje, Bw.
Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo.
Balozi
wa Jamhuri ya Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura (kulia) pamoja na
Afisa aliyeambatana na Mhe. Waziri Mushikiwabo wakifuatilia mazungumzo.
Wakati mazungumzo yakiendelea.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.
Wawekezaji wazawa wana haki kuwekeza kwenye gesi, mafuta
Na Greyson Mwase
Serikali imesema wawekezaji wazawa wana haki ya kuwekeza kwenye
sekta za mafuta na gesi ili sekta hizo ziwe na mchango mkubwa katika
ukuaji wa uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa na mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya
Nishati na Madini Mhandisi Petro Marwa kwenye maonesho ya
kimataifa ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Petro alisema kumekuwepo na dhana kuwa wawekezaji
kutoka nje ya nchi wanapewa kipaumbele katika uwekezaji kwenye gesi
na mafuta jambo ambalo si sahihi.
Alisema ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania ananufaika na uwekezaji
kwenye sekta za gesi na mafuta, Serikali imeweka sheria nzuri za
kuwezesha watanzania kuwa sehemu ya uchumi wa gesi na mafuta.
“ Kwa mfano Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 kifungu cha 218
kinaeleza ushiriki wa serikali kupitia Kampuni ya Mafuta ya Taifa
(National Oil Company) na kifungu cha 219 na 220 kinaainisha ushiriki
wa watanzania katika utoaji wa huduma na bidhaa kwa makampuni
yaliyowekeza nchini kwenye sekta za mafuta na gesi,” alisema
Mhandisi Petro.
Mhandisi Petro aliendelea kusema kuwa serikali imeweka mikakati
mbalimbali kuhakikisha watanzania wanakuwa si watazamaji kwenye
uvunaji wa rasilimali za gesi na mafuta bali wanakuwa ni washiriki kamili
na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Akielezea mikakati hiyo, Mhandisi Petro alisema kuwa Serikali kupitia
Wizara ya Nishati na Madini ilianzisha kozi mbalimbali zinazohusu
mafuta na gesi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Madini (MRI).
Aliongeza kuwa Wizara imekuwa ikiwezesha wanafunzi wanaofanya
vizuri katika masomo ya sayansi kupata ufadhili wa kusomea masuala
ya mafuta na gesi katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Mhandisi Petro alitoa wito kwa watanzania wote kuchangamkia fursa
zilizopo katika sekta za mafuta na gesi ili nchi iweze kutoka kwenye
kundi la nchi masikini duniani na kuingia katika orodha ya nchi zenye
kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa
inavyofafanua.
Afisa Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kulia) kutoka Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu
yanavyochenjuliwa kwa mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo
kwenye banda la TMAA katika maonesho hayo.
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo (kushoto)
akielezea majukumu ya Wizara kwa mteja aliyetembelea banda hilo
katika Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es Salaam
International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki kutoka Kampuni ya Kuendeleza Nishati ya Jotoardhi Tanzania
(TGDC) wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Maonesho ya Kimataifa
ya Saba Saba (Dar es Salaam International Trade Fair)
yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Mmoja wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika
la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba
Saba (Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika
picha ya pamoja kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba (Dar es
Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika Viwanja vya
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Neema Mwambenja kutoka Taasisi ya Environmental Foundation for
Tanzania (EFFORT) ambayo ni mdau wa Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) (katikati) akitoa maelezo ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo
kwenye banda la REA, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba
(Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Odriana
Magige kutoka taasisi hiyo.
Mhandisi Migodi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Suleiman
Khalid (katikati) akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
Kushoto ni Afisa Usalama na Mazingira kutoka shirika hilo Paul Thobias.
Banda la Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi zake kama
linavyoonekana pichani kwenye kwenye Maonesho ya Kimataifa ya
Saba Saba (Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea
katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari, Mhandisi Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini
Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa
Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza
kuwahudumia wateja katika Maonesho ya Kimataifa ya Saba Saba
(Dar es Salaam International Trade Fair) yanayoendelea katika
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wednesday, June 29, 2016
Shambulio katika uwanja wa ndege lauwa watu 41 Istanbul
Washambuliaji
wa kujitowa muhanga wamewauwa zaidi ya watu 41 na kujeruhi wengine 140
katika shambulio dhidi ya uwanja wa ndege wa Ataturk mjini Istanbul
katika mfululizo wa miripuko ya mabomu dhidi ya Uturuki.
Idadi ya
watu waliouwawa katika shambulio la uwanja wa ndege wa Istanbul
imeongezeka na kufikia 41. Awali Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yidirm
amesema watu 36 wameuwawa hapo jana wakiwemo washambuliaji watatu wa
kujitowa muhanga ambao waliwasili katika uwanja wa ndege huo kwa kutumia
taxi na kujiripuwa mara tu baada ya kuanza kufyatuwa risasi.Waziri wa
sheria wa Uturuki Bekir Bozdag amesema watu 147 wamejeruhiwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege huo baada ya kutokea kwa
shambulio hilo hapo jana Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yidrim amesema
kundi la Dola la Kiislamu linaonekana kuhusika na shambulio hiilo
Binali
amesema "Uchunguzi wa vikosi vyetu vya usalama unaashiria kwamba
shambulio hilo la kigaidi limetekelezwa na kundi la Daesh na licha ya
kwamba uchunguzi unakielekezea kidole kundi hilo la Dola la Kiislamu
uchunguzi huo bado unaendelea.Uwanja wa ndege unafunguliwa tena kwa
safari saa nane usiku na safari za ndege zitarudi katika hali ya
kawaida."
Kwa
mujibu wa maafisa polisi ilifyatuwa risasi kujaribu kuwazuwiya
washambuliaji wawili kabla hawajafika kituo cha ukaguzi wa usalama
katika ukumbi wa kuwasili abiria katika uwanja wa ndege huo lakini
waliripuwa mabomu yao. Afisa wa Uturuki amesema wengi waliouwawa
walikuwa ni raia wa Uturuki lakini pia kuna wageni miongoni mwa watu
waliouwawa.
Shambulio lafanana na la Brussels
Shambulio
hilo kwa kiasi fulani linafanana na shambulio la kujitowa muhanga
lililofanywa na wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu katika uwanja wa
ndege wa Brussels hapo mwezi wa Machi na kuuwa watu 16 kabla ya
shambulio jengine kuuwa watu wengine 16 siku hiyo hiyo katika njia ya
reli ya chini ya ardhi katika mji mkuu huo wa Ubelgiji.
Mashahidi
walirepoti kusikia milio ya risasi kutoka sehemu mbali za uwanja wa
ndege huo wa Atartuk ambao ndio uwanja wa ndege mkubwa kabisa nchini
Uturuki na wa tatu kwa kuwa na harakati kubwa za safari za kimataifa
barani Ulaya.
Rais Recep Tayyip Erdogan amelani shambulio hilo la kigaidi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.
Uwanja wafunguliwa tena
Ndege
tayari zimeanza kutuwa tena katika uwanja wa ndege huo leo ajafiri baada
ya uwanja wa ndege huo kufungwa kabisa kwa masaa kadhaa hapo jana
kufuatia shambulio hilo la kigaidi.Mamia ya safari zilifutwa kufuatia
shambulio hilo.
Shirika
la ndege la Uturuki ambalo limefuta zaidi ya safari 340 limekuwa
likiwarejeshea abiria fedha zao au tiketi mbadala lakini bado kuna
mkanganyiko kwa wasafiri wengi.
Shambulio
hilo la jana ni baya kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa zaidi ya
muongo mmoja mjini Istanbul.Kundi la Dola la Kiislamu limekuwa
likilaumiwa kwa kuhusika na mashambulio kadhaa nchini Uturuki katika
kipindi cha mwaka mmoja uliopita.DW
LAPF NDANI YA MAONESHO YA SABASABA 2016
Mkuu wa
Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James
Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sababu za ushiriki wa
Mfuko katika maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).
Afisa
Mifumo ya kompyuta kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yohana Nyabili
akitoa maelezo kwa mwanachama wa Mfuko pamoja na kumpatia taarifa ya
michango yake mara baada ya mwanachama huyo kutembelea banda ya Mfuko
kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa (Saba Saba 2016).(P.T)
PBZ YAADHIMISHA SHEREHE ZA MIAKA 50 KWA KUSAIDIA JAMII NA KUTEMBELEA HOSPITALI YA KIDONGOCHEKUNDU.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akimkabidhi msaada wa magodoro 100
Kamishna Msaidizi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Omar Salum Mgaza. hafla
hiyo imefanyika katika viwanja vya Mafunzo Kilimani Zanzibar.
Baadhi
ya magodoro 100 yaliotolewa msaada na PBZ kwa ajili ya matumishi ya
Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar, ikiwa ni kusherehekea miaka 50
ya PBZ Zanzibar. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Chuo cha
Mafunzo Kilimani Zanzibar.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ akizungumza na Maofisa wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar
wakati wa kikabidhi msaada wa magodoro kwa ajili ya Wanafunzi wa Chuo
cha Mafunzo Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mafunzo
Kilimani Zanzibar.
Kamishna
Msaidizi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Omar Salum Mgaza akitowa shukrani
kwa PBZ kwa msaada wao huo wa magodoro umeletwa wakati muafaka na
kuwata taasisin nyengine kujitokeza kutoa misaada.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ Ndg.Juma Ameir akisalimiana na Muuguzi Dhamana wa
Hospitali ya Kidongochekundu Zanzibar Ndg. Haji Vuai Hilal, wakati
walipofika katika hospitali hiyo ya Mental kutowa misaada ya mashuka 200
kwa ajili ya hospitali hiyo. katikatika Afisa Masoko wa PBZ Ndg.
Mohammed Nuhu.
Afisa
Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akisalimiana na Muuguzi Dhamana wa
Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar Haji Vuai Hilal.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ Juma Ameir akizungumza na Uongozi wa Hospital ya Mental
Kidongochekundu Zanzibar wakati wa kutembelea hospitali hiyo na kutoa
msaada wa mashuka 200 ikiwa ni kusherehekea miaka 50 ya PBZ Zanzibar
hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hospitali hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akikabodhi msaada wa mashuka kwa ajili
ya hospitali ya Mental Kidogochekundu Zanzibar akipokea msaada huo
Muuguzi Dhamani wa hospitali hiyo Ndg Haji Vuai Hilal. ikiwa ni
kusherehekea miaka 50 ya PBZ kushaidia jamii Zanzibar.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akikabodhi msaada wa mashuka kwa ajili
ya hospitali ya Mental Kidogochekundu Zanzibar akipokea msaada huo
Muuguzi Dhamani wa hospitali hiyo Ndg Haji Vuai Hilal. ikiwa ni
kusherehekea miaka 50 ya PBZ kushaidia jamii Zanzibar.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir akimkabidhi mmoja wa mgonjwa katika
hospitali hiyo Bi Amina Mwinyi msaada wa tende kwa ajili yao katika
kipindi hichi cha mfungo wa mwezi wa ramadhani.
Mmmoja
wa mgonjwa katika hospitali Bi Amina Mwinyi, hiyo akitowa shukrani kwa
niaba ya wezake kwa uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo kwao na kuuthamini
na kuwataka na Wananchi wengi kujitokeza kuwasaidia kwa vitu
mbalimbali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir akikabidhi msaada wa tenda mmoja wa
wagonjwa wa hospitali hiyo Ndg. Mrisho Idrisa Hussein.
Muuguzi
Dhamana wa Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar Ndg Omar Vuai
Hilal akitowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ na Wafanyakazi wao kwa msaada
wao huo katika hospitali hiyo.
Wafanyakazi
wa PBZ wakijumuika na Mkurugenzi Mtenda wa PBZ Ndg Juma Ameir katika
kutoa huduma kwa wateja ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 50 ya
PBZ tangu kuazishwa kwa benki hiyo wakiwa katika Tawi la Malindi
Zanzibar.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Ameir akitowa huduma kwa
Wateja wa PBZ katika tawi la PBZ Malindi, Pbz imetimisha miaka 50 tangu
kuazishwa kwa kwake Zanzibar.
Wateja wa PBZ wakipita huduma za Kibenki katika Tawi la PBZ Malindi Zanzibar.
Meneja
wa Benki ya Watu wa Zanzibar Tawi la Malindi akitowa huduma kwa wateja
wao akiwa na Afisi wa PBZ wakati wa shamrashamra za kusherehekea miaka
50 ya PBZ Zanzibar.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akitowa zawadi kwa Wateja wa PBZ ikiwa
ni shamrashamra za kusherehekea miaka 50 ya PBZ kuazisha kutowa huduma
za Kibenki Zanzibar.
Wateja wa PBZ wakiwa katika Tawi la Malindi Zanzibar wakisubiri kupata huduma za Kibenki katika tawi hilo.
Wateja wakipatya huduma katika Benki hiyo Tawi la Malindi Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ akitowa zawadi kwa wateja wa PBZ Tawi la Malindi Zanzibar.
Mteja
wa PBZ Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma
za Kibenki, wakati wa shamrashamra hizo za kusherehekea miaka 50 ya PBZ
na kuwataka kuboresha zaidi huduma zao kwa wateja.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PBZ akizungumza na waandishi wa habari malengo na
changamoto za PBZ kwa wateja wake na malengo yao kutowa huduma kwa
Wateja wao na kuboresha zaidi huduma zao.
Afisa
wa PBZ Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar Ndg Jaha akitowa huduma za kibenki
kwa Wateja wao katika tawi hilo PBZ inatimiza miaka 50 tangu kuazishwa
kwake.
Afisa
Manunuzi wa PBZ Bi Mwanaidi Ramadhani akitowa huduma za Kibenki kwa
Wateja wa PBZ Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar, Maofisa wa PBZ wameungana
na wafanyakazi wa Matawi la PBZ kutowa Huduma za Kibenki kuadhimisha
miaka 50 ya PBZ tangu kuazishwa kwake.
Meneja
wa PBZ Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar akitowa huduma za Kibenki kwa
Wateja wa PBZ ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea miaka 50 ya PBZ
Zanzibar.
Meneja
wa PBZ Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa shamrashamra za kutimia miaka 50 ya PBZ Zanzibar.
Afisa
manunuzi wa PBZ Bi Mwanaidi Ramadhani akitoa zawadi kwa Wateja wa PBZ
Tawi la Mwanakwerekwe Zanzibar ikiwa ni kuadhimisha miaka 50 ya PBZ
tangu kuazishwa kwake mwaka 1966-2016
Mteja
wa PBZ akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma za PBZ ni
nzuri na kuwataka kuziboresha zaidi katika kipindi kijacho kwa wateja
wao na kuwataka kuongeza huduma na ATM na kuziboresha zaidi huduma hizo
kuwafikia hadi wananchi wa vijiji kupata huduma hii ya ATM huko
mashamba.
Imetayarishwa na OthmanMapara.
Zanzinews.com
Subscribe to:
Posts (Atom)