TRA

TRA

Thursday, November 3, 2016

KUELEKEA MCHEZO WA WATANI WA JADI WA LONDON,MAJEMBE MANNE YAREJEA ARSENAL

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


_65364271_65364270
Kuelekea mchezo wa watani wa jadi katika jiji la London nchini England maarufu kama dabi ya London ya Kaskazini kati ya Arsenal watakaowakaribisha Tottenham Hotspurs katika uwanja wa Emirates siku ya Jumapili, wenyeji wa mchezo huo wamepata ahueni baada ya wachezaji wake wanne wa kikosi cha kwanza ambao walikuwa majeruhi kupata nafuu ya majeraha yao mna kwamba sasa wanaweza kujumuishwa katika katika kikosi kitachocheza mchezo huo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana leo zinaonyesha kuwa Theo Walcot, Sant Carzola, Hector Bellarin na Nacho Monreal ambao wote walikosekana katika mchezo uliopita wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Ludogorets Razgrad mbapo Arsenal walishinda kwa magoli 3-2 wakitokea nyuma baada ya kutanguliwa kwa mabao 2, wanarejea baada ya kuonekana afya zao zikiimarika.
Arsenal wamepoteza mchezo mmoja pekee toka ligi kuu ilipoanza baada ya kupoteza 4-3 dhidi ya Liverpool katika mechi yao ya ufunguzi wa ligi, na baadae kutoka sare na mabingwa watetezi Leicester City na timu ya Midlesbrough huku wakishinda mecchi zilizobaki na kufikisha pointi 23 pamoja na viongozi wengine wa ligi Manchester City na Liverpool.
Mechi ijayo ni muhimu kwa pande zote mbili kwa kuwa ni mechi ya watani wa jadi lakini pia ni mechi inayowapa nafasi kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi nchini England. Timu zote zinaonekana kufanya vizuri katika michezo yao na wachezaji wa Arsenal wanaorejea wamekuwa chachu ya kufanya vizuri kwa klabu yao ya Arsenal.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger