Matumaini ya
Muingereza Johanna Konta kufika fainali za Wimbledon yamefutiliwa mbali
baada ya kuchapwa na Venus Williams wa Marekani katika hatua ya nusu
fainali.
Venus mwenye miaka 37 alicheza kwa umakini mkubwa zaidi na kushinda kwa seti 6-4 6-2.
Konta
anayeshikilia nafasi ya sita kwa ubora duniani, alitegemea kufika
fainali hizo na kuwa wa kwanza kufanya hivyo kwa Uingereza tokea mwaka
1977. Matumaini pekee kwa Konta ni kuingia ndani ya tano bora kwa ubora.
Venus atachuana na Garbine Muguruza wa Hispania aliyemchapa Magdalena Rybarikova wa Slovakia kwa seti 6-1 6-1.
No comments:
Post a Comment