Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyesimama) akizungumza na
Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa juu ya mgogoro baina yao na pori
la akiba la Mkungunero katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (aliyesimama) akiwaonesha
Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa Naakala ya tangazo la Serikali
lililotangaza pori la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano wa kujadili
mgogoro baina ya wanachi hao na pori la akiba katikati ya Wiki (Juni 15,
2016).
Mkuu
wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Shaban Kissu (aliyesimama) akizungumza na
Wananchi wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa juu ya mgogoro baina yao na pori
la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa huo
katikati ya Wiki (Juni 15, 2016).
Mzee
Mathayo wa kijiji cha Ikengwa akiishukuru serikali ya Rais Magufuli kwa
kuanza kushughulikia mgogoro baina ya wananchi wa kijiji hiko na pori
la akiba la Mkungunero wakati wa mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa
Dodoma ambapo kamati iliyohusisha wananchi, Pori la akiba Mkungunero na
Uongozi wa Wilaya Kondoa iliundwa kumaliza mgogoro huo.
Baadhi
ya Viongozi wa Wilaya ya Kondoa, pori la akiba Mkungunero na Viongozi
wa kijiji cha Ikengwa kinachopakana na pori hilo wakiwa kwenye mkutano
wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma katikati ya Wiki ili
kujadili namna ya kutatua mgogoro baina ya wanachi wa kijiji hiko na
pori la Mkungunero.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (katikati) akiagana na Wananchi
wa Kijiji cha Ikengwa Kondoa baada ya kumaliza mkutano wa hadhara juu
ya mgogoro baina yao na pori la akiba la Mkungunero katikati ya Wiki
ambapo mkuu wa mkoa ameunda kamati ya kumaliza mgogoro huo inayohusisha
wananchi, Pori la Mkungunero na Uongozi wa Wilaya Kondoa na wananchi
wameshukuru makubaliano yaliyofikiwa ya kutafutiwa maeneo mengine ya
makazi, kilimo na mifugo (Juni 15, 2016).
Wakina
mama wa jamii ya kibarbaigi wa kijiji cha Ikengwa Kondoa wakimshukuru
Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana baada ya kufurahishwa na
makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa hadhara ya kutafutiwa maeneo
mengine ya makazi, kilimo na mifugo kwa lengo la kumaliza mgogoro wa
wananchi hao na pori la Mkungunero.
SHARE
No comments:
Post a Comment