Mama
Maria Tereza akisisitiza jambo wakati akitoa shukrani zake kwa wanawake
wa Tanzania wanaofanya miradi mbalimbali ya kupambana na mabadiliko ya
tabianchi.
MAKAMU
wa Rais mstaafu wa Hispania, Maria Tereza Fernandes de la Vega Sanz
(67), amesema kwamba amefurahishwa mno na mafanikio ya wanawake 15 wa
Tanzania katika kipindi kifupi baada ya mafunzo waliyoyapata jijini
Madrid mapema mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa chakula cha usiku alichowaandalia akinamama hao wanaotekeleza
mradi wa Green Voices katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam usiku
huu mara baada ya kutua kutoka Hispania, Mhe. Maria Tereza amesema
amefarijika kuona wazo lake lililoibuka mwishoni mwa mwaka 2015 la
kuwawezesha wanawake kupambana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko
ya tabianchi limeweza kuzaa matunda.
Mama Maria Tereza ndiye anayefadhili miradi hiyo kupitia taasisi yake ya Women for Africa Foundation.
Mama Maria Tereza Fernandes de la Vega Sanz (kushoto) akimkabidhi zawadi Balozi Getrude Mongella katika hafla hiyo.
“Ni
mwaka jana tu mwishoni nilipowaza namna ya kuwawezesha wanawake, hasa
wa Tanzania, katika vita ya dunia ya kupambana na mabadiliko ya
tabianchi, lakini nafarijika kusikia kwamba wanawake wachache ambao
tuliwapatia mafunzo nchini Hispania leo hii wameweza kufanikiwa kuliko
hata tulivyotarajia, ni muda mfupi na mafanikio ni makubwa,” alisema.
Mama
Maria Tereza alikuwa makamu wa rais wa Hispania kati ya Aprili 18, 2004
hadi Oktoba 20, 2010, na ndiye alikuwa msemaji wa serikali ya Waziri
Mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero. Yeye ni mwanamke wa kwanza kushika
nafasi hiyo katika historia ya Hispania.
Katika
hafla hiyo, Mratibu wa Mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Bi.
Secelela Balisidya, amesema kwamba ukiacha wanawake watano wanahabari,
wanawake 10 wanaotekeleza miradi mbalimbali wameweza kuwaelimisha
wanawake wengine 250 mpaka sasa ambao wako kwenye vikundi mbalimbali
katika mikoa sita ya Tanzania Bara.
Mama Mariam Bigambo (kulia) akimvisha mkufu wa shanga Mama Maria Tereza kama zawadi ya wanawake hao.
Bi.
Secelela amesema kwamba, mafanikio hayo yanatia moyo hasa kutokana na
serikali nayo kuunga mkono jitihada hizo za wanawake nchini.
“Kila
mradi unaonekana kuigusa jamii moja kwa moja na tunashukuru kuona
kwamba viongozi mbalimbali wa serikali wanaitikia na kuwaunga mkono
akinamama hawa,” alisema.
Kwa
upande mwingine, Dk. Sophia Mlote, ambaye anatekeleza mradi wa kilimo
endelevu cha nyanya (Green House) Kinyerezi jijini Dar es Salaam,
amesema changamoto pekee ni gharama za kuendesha miradi hiyo hasa mtaji
anzilishi, kwani ingawa akinamama wengi wanajifunza, lakini wanashindwa
kuanzisha kutokana na uwezo mdogo.
Ameiomba
serikali na wahisani kuangalia namna ya kuwawezesha akinamama hao na
jamii nzima kwa ujumla, huku akisisitiza kwamba, lengo siyo tu
kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, bali ni chanzo kikubwa cha ajira
kwa wanawake na taifa kwa ujumla.
Mama Maria Tereza akimkumbatia Balozi Mongella.
Mratibu wa Mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Bi. Secelela Balisidya, akieleza jambo wakati wa hafla hiyo.
Ana Salado (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Regina kwa niaba ya wanawake wa Tanzania.
Balozi Getrude Mongella (kulia) akifafanua jambo kwa Makama wa Rais mstaafu wa Hispania, Maria Tereza.
Baadhi
ya washiriki wa mradi huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Mama Edda
Sanga (wa pili kulia mstari wa mbele).
Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, Maria Tereza, akijisevia chakula.
Regina, mmoja wa washiriki wa miradi iliyo chini ya Green Voices, akipakua supu ya uyoga.
Akinamama wakiwa pamoja na wageni kutoka Hispania.
SHARE
No comments:
Post a Comment