SERIKALI inapoteza shilingi bilioni 18 kutokana na kukosa rada za
kuongezea ndege na kufanya nchi ya Kenya ipate mapato hayo kwa kuwa
rada.
Hayo ameyasema leo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani wakati wa Mkutano wa kwanza wa
Wamiliki wa Ndege wa Afrika Mashariki na Afrika (IATA), amesema kuwa
kutokana na Serikali kukosa mapato wameagiza rada mbili ambazo
zitagharimu dola za Kimarekani Milioni 24.
Ngonyani amesema kuwa
rada hizo mbili zitafungwa nusu ya anga la Tanzania ambazo
zitafanya serikali ya Tanzania kupata fedha kutokana na ndege
zitazotumia mawasiliano ya Rada kulipia ambapo kwa sasa hatuna uwezo
huo.
Amesema kuwa katika mkutano huo shirika la ndege Presion ndio
mwanachama wa IATA huku Shirika la Ndege za Serikali (ATCL) likikosa
sifa kuwa mwanachama kutokana ndege zake kushindwa kukidhia vigezo
vilivyowekwa.
Ngonyani amesema kuwa kutokana na mkakati wa serikali kwa sasa
wanatarajia kununua ndege mbili za kisasa na baadae kuongeza ndege
zingine katika kutoa huduma ya wananchi na kwenda hadi nje ya Afrika.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari amesema kuwa wanaendelea katika kuboresha huduma za anga.
Imeandaliwa na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin
Ngonyani akizungumza katika mkutano wa kwanza wa wamiliki wa ndege wa
Afrika mashariki na na Afrika kwa ujumla (IATA) jijini Dar es Salaam.
Pia katika mkutano huo wanaanalia changamoto mbalimbi katika sekta ya
usafiri wa Anga.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa
kwanza wa Wamiliki wa Ndege wa Afrika Mashariki na Afrika (IATA) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wa wadau na wamiliki wa ndege wakiwa katika
Mkutano wa kwanza wa Wamiliki wa Ndege wa Afrika Mashariki na Afrika (IATA) ulioanyika leo jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment