Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa (Kulia) akitoa maelezo ya
hali ya miundombinu ya mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea ofisini kwake.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa (Kulia)
wakati alipotembelea ofisini kwake kupata taarifa ya hali ya miundombinu
katika mkoa huo.
Meneja
wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Mbeya Eng. Paul
Lyakurwa (wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhusu barabara ya
Ikana-Makamba –Chitete kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) wakati alipokagua barabara
hiyo kwenye mkoa wa Songwe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa
Mbeya Eng. Paul Lyakurwa wakati alipokagua barabara ya Ikana-Makamba
–Chitete iliyopo mkoa wa Songwe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua
kituo cha kukuza mawimbi ampilification station kilichopo miangalau
mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Meneja wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
Mkoa wa Katavi na Rukwa Bw. Peter Kaguru.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Stephen akitoa taarifa ya hali ya Miundombinu
katika mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa wakati alipomtembelea ofisini kwake.
Meneja
wa Wakala wa barabara nchini (Tanroads) Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina
(wa pili kushoto) akisoma taarifa ya utendaji ya taasisi zilizo chini
ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Waziri Profesa Makame
Mbarawa wakati alipofanya mazungumzo na viongozi wa taasisi hizo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia) akizungumza na viongozi wa taasisi zilizo chini ya yake (hawapo
pichani), wakati alipokutana nao Mkoani humo.
Viongozi
wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mkoani Rukwa, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati alipokutana nao Mkoani
Rukwa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezitaka
taasisi zilizo chini ya Wizara yake kuanzisha mfumo maalumu wa
makubaliano utakaotumika kupima utendaji kazi wa watumishi ili kuweza
kufikia malengo yaliyokusudiwa na kutoa matokeo chanya.
Waziri
Mbarawa ameyasema hayo Mkoani Rukwa alipofanya mazungumzo na Viongozi
na watendaji wa taasisi hizo wakati alipotembelea mkoa huo kwa lengo la
kukagua hali ya miundombinu na kuwaeleza mtazamo mpya wa Serikali ya
Awamu ya Tano.
Amesema
katika mfumo huo Waziri ataingia mkataba na wenyeviti wa bodi wakati
Katibu Mkuu wa kila sekta kuingia mkataba na watendaji wakuu wa taasisi
hizo na watendaji hao wataingia mikataba na wafanyakazi wao ili kuweza
kuweka mazingira ya kila mfanyakazi kufikia malengo yaliyowekwa na
wizara pamoja na taasisi husika.
“Mimi
nitawekeana mkataba na wenyeviti wa bodi za taasisi zote, kwa Sumatra
moja ya vipengele vitakavyokuwa kwenye mkataba huo ni pamoja na mkakati
madhubuti wa kupunguza ajali za barabarani zinazosababisha vifo kwa
Watanzania, TCRA Makusanyo kwenye makampuni ya simu na taaasisi nyingine
hivyo hivyo”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha,
Waziri Mbarawa amehimiza taasisi hizo kufanya kazi kwa bidii ili
kuwajengea miundombinu iliyo bora watanzania ili kuweza kuwafikisha
katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Aidha,
Profesa Mbarawa amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa ubunifu, kasi
na uadilifu ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na
kuwajibika kwa ajili ya maslahi ya wananchi na kubadili maisha ya
watanzania kwa ujumla.
“Ni
wakati wa kutekeleza kauli mbiu ya hapa kazi tu kwa vitendo, hivyo
nawataka muwe wabunifu katika utendaji kazi za kila siku na muweze kutoa
matokeo chanya ya haraka kwa wananchi”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Awali
akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa, Profesa
Mbarawa amesema Serikali kupitia wizara yake itaendelea kupandisha hadhi
baadhi ya barabara zilizo chini ya Halmashauri na kuwa chini ya Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS), ili kuweza kuendelea kuboresha hali ya
miundombinu na kuunganisha mkoa huo na Mikoa ya Mbeya, Rukwa pamoja na
nchi zinazozunguka mikoa hiyo kwa barabara za lami.
Profesa
Mbarawa amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa huyo kuwa Serikali itaendelea
kufanya matengenezo kwa barabara zote nchini kupitia gawio kutoka Mfuko
wa Barabara nchini (Road fund) ili kuinua uchumi wa Mkoa.
Waziri
Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua utendaji kazi kwa wafanyakazi
pamoja na hali ya Miundombinu katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
SHARE








No comments:
Post a Comment