Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akipokea madawati 350 yenye thamani ya
shilingi milioni 58 kwa shule 12 za msingi katika wilaya ya Tabora,
kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ally Maswanya(kulia),
makabidhiano hayo yaliofanyika shule ya Msingi Mihayo iliyopo manispaa
ya Tabora jana.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ally Maswanya Akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi Mihayo mara baada ya makabidhiano hayo yaliofanyika shuleni hapo iliyopo manispaa ya Tabora jana.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mihayo waakifurahia madawati mara baada ya makabidhiano hapo shuleni
Julai
18 2016 Tabora: Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 350
yenye thamani ya shilingi milioni 58 kwa shule 12 za msingi katika
wilaya ya Tabora(50),Nzega(200) na Urambo(100) ikiwa ni mchango wa
kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa
madawati katika shule za msingi nchini.
Akizungumza
leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya msingi
Mwangoye katika manispaa ya Tabora, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa
Ally Maswanya amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya
kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo
nchini.
“Mchango
huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika
kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini
kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga
viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo
madaktari, wahandisi na wengineo, “amesema Maswanya.
Maswanya
amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika
shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya, Iringa, Morogoro, Dar
es Salaam, Mwanga na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa
madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.
Makabidhiano
yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora mheshimiwa Aggrey Mwanri ambaye
alisema madawati hayo 350 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa
watoto katika Mkoa wa Tabora na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga
mkono zoezi hilo.
“Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu
kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la
ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa
Tabora. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 350 yatawawezesha mamia
ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao
katika mazingira bora zaidi,” alisema Mwanri.
Madawati
hayo 350 yametolewa Tabora kwa shule za msingi 12 kama ifuatavo,
Mihayo,Kasela,Shigamba,Itobo,Mwamala,Mwangoye,Umoja,Urambo,Ukombozi,Ussoke,
Tulieni na Mabatini. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment