Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya
utangulizi kuhusu Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka
2014 katika uzinduzi wa matokeo hayo uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Naibu
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Watu wenye Ulemavu Dkt. Abdallah Possi akionyesha Ripoti ya Matokeo ya
Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014. Uzinduzi huu
umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango.
Mwakilishi
wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Azfar Khan akizungumza leo
jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa
Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014.
Baadhi viongozi waliohudhulia katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014.
Mwakilishi wa shirika la UNICEF, Cecilia Baldeh akizungumza na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014 iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
UTUMIKISHWAJI
wa Watoto bado ni tatizo kubwa nchini ambapo kati ya watoto watatu
wenye umri wa miaka 5 - 17, mtoto mmoja anafanya kazi ambazo ni
hatarishi katika maisha yake kiafya, kimwili na kisaikolojia.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa
Watoto Tanzania wa Mwaka 2014, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Dkt. Abdallah Posi amesema
tatizo la utumikishwaji wa watoto bado ni kubwa hapa nchini na hivyo ni
wajibu wa jamii kuwekeza katika elimu badala ya kuwaajiri au
kuwatumikisha watoto.
“Utumikishwaji
wa watoto bado ni tatizo kubwa duniani kote si Tanzania pekee, kwani
kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Kazi Duniani (ILO), asilimia 11 ya
watoto wote duniani (watoto milioni 264) wenye umri wa miaka 5 – 17
wanatumikishwa kwenye ajira za aina mbalimbali,” amesema Dkt. Posi.
Dkt.
Posi amesema kwa mujibu wa ripoti ya utumikishwaji wa watoto Tanzania
wa mwaka 2014/15, watoto wenye umri wa miaka 5 – 17, watoto milioni 4.2
ambao ni sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali za
kiuchumi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina
Chuwa amesema utafiti huu umebainisha kuwa, watoto wanafanya kazi zaidi
katika sekta za Kilimo, Misitu na Uvuvi ambazo zinaajiri asilimia 92.1
ya watoto wote wanaojishughulisha na shughuli za kiuchumi.
Dkt.
Chuwa ameongeza kuwa watoto hutumia zaidi ya nusu ya muda wao (asilimia
58.8) wa siku kujihudumia na usafi binafsi ambapo wasichana wameonekana
kutumia asilimia 59.2 na wavulana hutumia asilimia 58.3 kujihudumia.
Aidha,
shughuli za kujisomea kwa watoto ni asilimia 15.5 ambapo wavulana
wanatumia muda mrefu zaidi kujisomea kwa asilimia 16.4 na wasichana
hutumia asilimia 14.6 kujisomea.
SHARE
No comments:
Post a Comment