
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya kukabidhi
hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 6/-pamoja na T-shirt 60 kwa
Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko(katikati) jana kwa niaba ya
chama hicho kwa ajili ya ziara ya mafunzo kwa wahariri wa habari za
michezo Tanzania itakayofanyika Nairobi Kenya, kuanzia Julai 7 -11 mwaka
huu.Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni
hiyo, Jacquiline Materu.

Mkuu wa
kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline
Materu(kulia)akiongea na waandishi wa wa habari(hawapo pichani)wakati wa
hafla fupi ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni
6/-pamoja na T-shirt 60 kwa Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert
Mkoko(katikati)jana kwa niaba ya chama hicho kwa ajili ya ziara ya
mafunzo kwa wahariri wa habari za michezo Tanzania itakayofanyika
Nairobi Kenya, kuanzia Julai 7 -11 mwaka huu.Kushoto ni Meneja Uhusiano
wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu.

Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akishuhudia Mkuu wa
kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline
Materu(kulia)akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert
Mkoko(katikati) moja ya t-shirt kati ya 60 zilizokabidhiwa pamoja na
hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 6/- jana kwa chama hicho kwa
ajili ya ziara ya mafunzo kwa wahariri wa habari za michezo Tanzania
itakayofanyika Nairobi Kenya, kuanzia Julai 7 -11 mwaka huu.

Makamu
Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko(kushoto)akipokea hundi yenye thamani
ya shilingi Milioni 6/- pamoja na t-shirt 60 toka kwa Mkuu wa kitengo
cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Jacquiline
Materu(kulia)jana kwa niaba ya chama hicho kwa ajili ya ziara ya mafunzo
kwa wahariri wa habari za michezo Tanzania itakayofanyika Nairobi
Kenya, kuanzia Julai 7 -11 mwaka huu,Katikati ni Meneja Uhusiano wa
kampuni hiyo, Matina Nkurlu.
Kampuni
ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo ndiyo wadhamini wakuu wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Jana imekabidhi hundi ya kitita cha
Shilingi Milioni 6/- kwa ajili ya kudhamini ziara ya mafunzo kwa
wahariri wa habari za michezo Tanzania itakayofanyika Nairobi, Kenya
kuanzia Julai 7 -11 mwaka huu.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari jana, Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu, alisema wao
wakiwa wadau wakubwa wa michezo nchini wameona ni fursa njema kusaidia
katika ziara hiyo.
Ziara
hiyo ya mafunzo imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habariza Michezo
Tanzania (TASWA) kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa
HabarizaMichezo Kenya (SJAK), ambapo wahariri 30 kutoka vyombo
mbalimbali vya habari nchini watashiriki.
“Vodacom
Tanzania tunaunga mkono juhudiza TASWA katika kuwajengea uwezo wahariri
wa habari za michezo na tunaamini watajifunza mengi kutoka kwa wenzao na
watakuja kuyatumia mafunzo hayo katika vyombo vyao vya habari na
kuwasaidia pia waandishi chipukizi wa habari za michezo,” alisema
Materu.
Alisema
kampuni yakeimetoa Shilingi Milioni 6/- kufanikisha ziara hiyo na pia
itatoa fulana maalum ambazo zitavaliwa na wahariri hao wakiwa huko.
Kwa
upande wake Makamu Mwenyekitiwa TASWA, Egbert Mkoko, aliishukuru Vodacom
Tanzania kwa udhamini wao na kuomba kampuni nyingine zisaidie kuwaunga
mkono.
“Vodacom
Tanzania wameonesha ni ndugu zetu wadamu, licha ya maombi yetu ya muda
mfupi kwao, lakini wametuchangia kiasi cha kutosha. Bajeti yetu bado
kubwa sana kwa ziara hii, milango ipo wazi kwa wengine watusaidie,”
alisema Mkoko, ambaye pia ni Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi
wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Kwa
mujibu wa Mkoko katika ziara hiyo, wahariri wa habari zamichezo wa
Tanzania watapata fursa ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari vya
Kenya na kubadilishana mawazo na wenzao wa Kenya kuhusiana na utendaji
kazi wao.
Pia
alisema kutakuwa na kongamano lililoandaliwa na SJAK jijini Nairobi na
litahusisha watoa mada kutoka Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa
Habari za Michezo (AIPS) chenye makao makuu yake Lausanne, Uswisi,
ambalo pamoja na mambo mengine litajadili umuhimu wa waandishi wa habari
katika kupromoti michezo.
“TASWA
inaamini hii ni ziara muhimu kwa wahariri wahabari za michezo nchini na
itasaidia kuboresha utendaji kazi wao,” alisema Mkoko na kuongeza kuwa
pia wahariri hao watashiriki michezo na wenzao wa Kenya.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment