TRA

TRA

Saturday, July 16, 2016

WAKULIMA ARUMEMERU WALALAMIKIA WACHAKACHUAJI WA MBEGU

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !




Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mbegu ya SEEDCO Kanda ya Kaskazini Daniel Mwambugi akitoa maelezo juu ya Mbegu za mahindi za kampuni hiyo zinazostahimili ukame na kumuwezesha mkulima kupata mavuno mengi katika shamba darasa lilipo kata ya King`ori wilaya ya Arumeru mkoani Arusha


Akiwaonyesha wananchi ambao ni wakulima waliouthuria shamba darasa la kampuni hiyo.Habari picha na Woinde shizza,Arusha


Wakulima wa Kijiji cha King`ori wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wamelalamikia baadhi ya wafanyabiashara wanaochakachua mbegu na kuwauzia wakulima mbegu feki zinazochangia kuzorota kwa kilimo na kuwakwamisha wakulima.

Wakulima hao Peter Kessy na Kanankira Mbise wamesema kuwa mavuno machache yaliyopatikana katika msimu huu wa mavuno yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na mbegu feki ,mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kupanda kwa bei ya pembejeo.

Wakizungumza katika shamba darasa lililoandaliwa na kampuni ya Mbegu ya Seedco wamesema kuwa tatizo la mbegu feki ,dawa feki na mbolea feki limekua likiwaumiza wakulima wengi kutokana na uelewa mdogo walionao juu ya pembejeo na matumizi yake.Diwani wa kata ya King`ori Peter Kessy anapendekeza kuwepo na vituo maalumu cha uuzaji wa mbegu katika vijiji na kata ili kuepuka tatizo la uchakachuaji wa mbegu linalowaathiri wakulima wengi.

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mbegu ya SEEDCO Kanda ya Kaskazini Daniel Mwambugi amesema kuwa kampuni hiyo inayosambaza mbegu bora za mahindi na mboga mboga imekua ikiingia mikataba na wasambazaji wa mbegu ili kuzuia uchakachuaji pia kuna alama ya utambuzi ambayo hutumika kutambua mbegu hizo hivyo amewataka wakulima kuwa makini katika ununuaji wa mbegu.


“Tunawashauri wakulima watumie mbegu zinazoendana na hali ya tabia ya nchi katika maeneo husika ili waweze kupata mavuno bora ,tunazo mbegu za muda mrefu na muda mfupi lakini pia tunawahamasisha kutumia mbegu bora ambazo ni Seedco ili waweze kuvuna kwa wingi” Alisema Daniel

Meneja wa Seedco upande wa mbegu za Mboga mboga Joyce Mbise alisema kuwa kampuni hiyo imeanza kusambaza mbegu hizo tangu mwaka jana hivyo ni fursa kwa Watanzania kuchangamkia kilimo cha mboga mboga ili waweze kukuza kipato cha mkulima na kuboresha lishe ya familia.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger